Vigezo vya Huduma vya Paxful Stablecoin

Tarehe ya kuanza: Machi 4, 2021

TAFADHALI SOMA MAKUBALIANO HAYA KWA MAKINI. Kwa kutumia huduma ya Paxful Stablecoin, unakubali kujifunga na makubaliano haya ya "Vigezo vya Huduma vya Paxful Stablecoin" na unatambua na kukubali kwamba umesoma kwa makini na kwa kina, umeelewa, na umekubali vigezo na masharti yote yanayojumuishwa humu, ambayo ni nyongeza ya Vigezo vya Huduma vya Paxful ("Makubaliano"). Vigezo vyovyote vilivyo katika herufi kubwa vilivyotumiwa lakini havijafafanuliwa hapa chini vina maana zilizoelezwa katika Makubaliano. Kama kukotokea mgogoro wowote kati ya Makubaliano na Vigezo vya Huduma vya Paxful Stablecoin wakati wa au kuhusiana na matumizi yako ya huduma ya Paxful Stablecoin, basi makubaliano Vigezo vya Huduma vya Paxful Stablecoin yatatumiwa.

Kuhusu Paxful Stablecoin

Huduma ya Paxful Stablecoin iko katika mfumo wa ushirikishi unaokuruhusu wewe, mtumiaji uliyethibitishwa wa Paxful, kuingia kwenye uchuuzi wa mwenzi kwa mwenzi kwa kampuni nyingine iliyochaguliwa awali ("Mshirika wa Stablecoin"), iliyochaguliwa na Paxful, kwa ajili ya ubadilishaji wa Bitcoin yako ili upate kiasi cha stablecoin chenye thamani inayolingana na USD, na kuhifadhiwa na Mshirika wa Stablecoin kwa manufaa yako. Kupitia muundo huu, Paxful Stablecoin inakuruhusu kuondoka kwenye nafasi ya Bitcoin yako hadi kwa stablecoin iliyochaguliwa.

Mfumo wa Ushirikishi

Huduma ya Paxful Stablecoin ni mfumo wa ushirikishi wenye lengo mahususi inayopatikana kwenye jukwaa la Paxful. Baada ya kuonyesha uhitaji wa kufanya miamala ya Paxful Stablecoin, Paxful itakuunganisha wewe kwa Mshirika wa Stablecoin kwa ajili ya utaratibu wa muamala. Kisha unapaswa kufuata maelekezo yanayotolewa ili uweze kuwasilisha vigezo vya ofa yako kwa Mshirika wa Stablecoin. Kampuni ya Stablecoin ikikubali vigezo vya ofa yako, miamala itafanywa kati yako na Mshirika wa Stablecoin. Kulingana na miamala ya msingi inayofanyika katika soko lake, Paxful haitaingilia, kudhibiti, kuwa na nguvu, usiri, au mamlaka katika miamala ya Paxful Stablecoin yanayoingiwa au kufanywa kati yako na Mshirika wa Stablecoin. Paxful haitalinda stablecoin zozote au kumshauri au kumwongoza mtumiaji yeyote wa Paxful kupata stablecoin hizo.

Mshirika wa Stablecoin anaweza kuwa na vigezo na masharti yake ya huduma ya miamala ya Paxful Stablecoin, na huduma ya Paxful Stablecoin inaweza kutofautiana katika viwango vya ubadilishaji, kasi ya ubadilishaji, na vigezo na masharti mengine ya nayowekwa na Mshirika wa Stablecoin ("Vigezo vya Mshirika wa Stablecoin"). Kwa kuingia katika muamala na Mshirika wa Stablecoin unakubali kujifunga na Vigezo vya Mshirika wa Stablecoin. Vigezo vya Mshirika wa Stablecoin ni halali isipokuwa katika hali vinapokiuka au kutofautiana na Makubaliano, Vigezo hivi vya Huduma vya Paxful Stablecoin, kama ni kinyume na sheria, havikubaliki au ni vigumu kuvifuata (kama inavyotolewa na maamuzi binafsi ya Paxful), au ikiwa wewe na Paxful Stablecoin mnaidhinisha kubadili Vigezo vya Mshirika wa Stablecoin. NI WAJIBU WAKO KUSOMA KWA MAKINI VIGEZO VYA MSHIRIKA WA STABLECOIN NA KUVIFUATA. IKIWA HAUTAFUATA VIGEZO VYA MSHIRIKA WA STABLECOIN, MIAMALA YAKO INAWEZA KUKATALIWA. KAMWE USIINGIE KATIKA MAUZIANO YA PAXFUL STABLECOIN ISIPOKUWA UMEFUATA VIGEZO NA MASHARTI YOTE YALIYOORODHESHWA. IKIWA UTASHINDWA KUFUATA VIGEZO NA MASHARTI HAYA, PAXFUL HAITAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA MCHAKATO WA MASHTAKA YA KUREJESHA FEDHA ZAKO.

Ada

Paxful itakuwa wazi siku zote kuhusu ada zetu. Ada zozote zitatumika kwenye matumizi ya huduma za Paxful. Kwa maelezo zaidi na masasisho ya viwango vya ubadilishaji, tafadhali rejelea Kituo cha Msaada.

Akaunti Zinazostahili na Maeneo Yaliyo na Vizuizi

Huduma ya Paxful Stablecoin inapatikana kwa watumiaji wanaotimiza matakwa ya huduma tu. Ili kutimiza matakwa ya kutumia huduma ya Paxful Stablecoin, unapaswa kuthibitisha akaunti yako na kuwa na angalau Bitcoin zenye thamani ya USD $1.00 kwenye pochi yako ya Paxful, pamoja na kiasi cha nyongeza cha Bitcoin kinachohitajika kwa ajili ya kulipia ada. Paxful ina haki ya kuzuia au kufanya marekebisho ya huduma ya Paxful Stablecoin kwa mtumiaji yeyote wa Paxful, na Mshirika wa Stablecoin anaweza kukataa muamala wowote na mtumiaji wa Paxful. Mbali na Maeneo yenye Vizuizi kama ilivyoainishwa kwenye Sehemu ya 2.7 ya Vigezo vyetu vya Huduma, huduma ya Paxful Stablecoin haipatikani kwa watumiaji wanaoishi katika Jimbo la Texas.

HAKUNA DHAMANA, KIMA CHA WAJIBU & KUKUBALI HATARI

HUDUMA ZA PAXFUL STABLECOIN ZINATOLEWA KATIKA MSINGI WA "KAMA ILIVYO" NA "KAMA INAVYOPATIKANA" BILA UDHAMINI, UWAKILISHI AU DHAMANA YOTOTE IWE NI KWA MAELEZO, MADOKEZO AU YA KISHERIA. KWA KIASI CHOTE KINACHORUHUSIWA NA SHERIA INAYOTUMIKA, PAXFUL INAKANUSHA UDHAMINI WOWOTE WA CHEO, UCHUUZI, UKAKAMAVU KWA KUSUDI MAALUM NA/AU UKIUKAJI. PAXFUL HAIFANYI UWAKILISHI WOWOTE AU UDHAMINI UNAOFIKIA TOVUTI, SEHEMU YOYOTE YA HUDUMA, NYARAKA ZOZOTE ZILIZOJUMUISHWA HAPA, ZITAKUWA ENDELEVU, ZISIZOINGILIWA, KWA WAKATI, AU ZISIZO NA DOSARI. PAXFUL HAITAWAJIBIKA KWA KUSHINDWA KWA PROGRAMU AU TEKNOLOJIA YA MSHIRIKA, USUMBUFU WOWOTE AU UPOTEVU ANAOWEZA KUKUMBANA NAO MTUMIAJI. UNATAMBUA NA KUKUBALI KWAMBA HUJATEGEMEA KAULI AU UELEWA MWINGINE, UWE WA MAANDISHI AU WA MDOMO, KUHUSIANA NA MATUMIZI YAKO YA HUDUMA NA TOVUTI. PASIPO KUWEKA KIMA CHA MWENDELEZO UNATAMBUA NA KUKUBALI HATARI ZOZOTE ZINAZOTOKANA NA KUTUMIA SARAFU ZA KIDIJITALI IKIJUMUISHA HATARI ZA KISHERIA, HITILAFU ZA NYENZO, MATATIZO YA PROGRAMU, KUSHINDWA KUUNGANISHA MTANDAO WA INTANETI, PROGRAMU ZISIZO SALAMA, MUINGILIANO WA MSHIRIKA MEINGINE, UNAOPELEKEA UPOTEVU AU KUSHINDWA KUFIKIA AKAUNTI AU POCHI YAKO NA DATA ZINGINE ZA MTUMIAJI, KUSHINDWA KWA SEVA AU UPOTEVU WA DATA. UNAKUBALI NA KUTAMBUA KWAMBA PAXFUL HAITAWAJIBIKA KWA KUSHINDIKANA KWA MUUNGANISHO, UVURUGAJI, HITILAFU, UHARIBIFU AU UCHELEWESHAJI UNAOWEZA KUKABILIANA NAO UNAPOTUMIA HUDUMA,VYOVYOTE UNAVYOWEZA KUSABABISHWA.

PAXFUL, WASHIRIKA NA WATOA HUDUMA WAKE, AU MAOFISA, WAKURUGENZI, MAWAKALA, WAFANYAKAZI, WASHAURI AU WAWAKILISHI, KWA NAMNA YOYOTE HAWATAWAJIBIKA KWA (A) KIASI CHOCHOTE KILICHO KIKUBWA KULIKO THAMANI YA JUMLA YA ADA INAYOLIPWA NA WEWE KWA AJILI YA HUDUMA AMBAYO INATOLEWA KATIKA MIEZI KUMI NA MBILI (12) KABLA YA KUTOKEA KWA UPOTEVU (B) KWA FAIDA YOYOTE ILIYOPOTEA, KUPUNGUA THAMANI AU FURSA YA BIASHARA, UPOTEVU, UHARIBIFU WOWOTE, RUSHWA AU UVUJAJI WA DATA AU MALI NYINGINE YOYOTE ISIYOSHIKIKA AU UHARIBIFU WOWOTE WA BAHATI MBAYA, USIO WA MOJA KWA MOJA, USIOSHIKIKA, AU WA MATOKEO YA MADHARA, IWE NI KULINGANA NA MKATABA, UHARIBIFU, UZEMBE, WAJIBU, AU UNAOTOKANA NA AU KULINGANA NA MATUMIZI YALIYOIDHINISHWA AU YASIYOIDHINISHWA YA WAVUTI AU HUDUMA, AU MAKUBALIANO HAYA, HATA KAMA MWAKILISHI WA PAXFUL ALIYEIDHINISHWA AMESHAURIWA AU ALIJUA AU ALIPASWA KUJUA UWEZEKANO WA UHARIBIFU HUO, NA PAMOJA NA HAYO KUSHINDWA KWA TIBA ILIYOKUBALIWA AU NYINGINE KWA KUSUDI LAKE, ISIPOKUWA KWA KIASI CHA HUKUMU YA MAHAKAMA AMBACHO UHARIBIFU HUO ULIKUWA MATOKEO YA UZEMBE WA PAXFUL, UDANGANYIFU, UTOVU WA NIDHAMU AU UKIUKAJI WA KUKUSUDIA WA SHERIA. BAADHI YA MAMLAKA HAZIRUHUSU UONDOLEWAJI AU KIMA CHA UHARIBIFU WA BAHATI MBAYA AU KUTOKUSUDIA, HIVYO KIMA CHA HAPO JUU VINAWEZA VISIKUHUSU WEWE.