VIGEZO VYA HUDUMA vya Paxful Inc.

MAKUBALIANO HAYA YANA MAELEZO MUHIMU ZAIDI KUHUSIANA NA HAKI NA MAJUKUMU YAKO, PAMOJA NA MASHARTI, VIKOMO NA HALI AMBAZO HAZIJAJUMUISHWA AMBAZO ZINAWEZA KUTUMIKA KWAKO. TAFADHALI YASOME KWA MAKINI.

Vigezo hivi vya Huduma na marekebisho na taarifa zozote mpya vinavyorejelewa hapa kama (“Makubaliano”) vinatengeneza makubaliano ya kisheria yanayoshughulikia utoaji wa huduma unayopata kwenye Paxful, ikiwa ni pamoja na utoaji wa soko ili kuwezesha wanunuzi na wauzaji wa “Mali Dijitali” (neno kama hilo linapaswa kueleweka kwa upana kuwa linajumuisha sarafu za dijitali kama vile Bitcoin, Tether na nyinginezo, zinazotumika na pochi ya Paxful) washirikiane pamoja katika shughuli za ununuzi na uuzaji (“Soko”), utoaji wa huduma za pochi dijitali, kushikilia na kuachilia Mali Dijitali jinsi inavyoagizwa baada ya kukamilisha ununuzi wa Mali Dijitali na huduma nyingine zozote zilizobainishwa katika Makubaliano haya (kwa ujumla “Huduma” na kwa umoja, “Huduma”) zinazotolewa na Paxful, Inc. na washirika wake wote, ikiwa ni pamoja na, wala si tu Paxful USA, Inc.(kwa ujumla, “Paxful” au “sisi” au “nasi” au “kampuni”) kwako kama mtu binafsi (anayerejelewa pia kama “mtumiaji” au “wewe”). Paxful.com na Huduma zake zinazohusiana vinamilikiwa na kuendeshwa na Paxful. Matumizi yako ya Huduma yatasimamiwa na Makubaliano haya, pamoja na Sera yetu ya Faragha, Sera ya Vidakuzi na Idhini ya Sahihi ya Kielektroniki.

VIGEZO HIVI VINAHITAJI MATUMIZI YA UPATANISHI ILI KUSULUHISHA MIZOZO BADALA YA KESI ZA MAHAKAMANI AU KUCHUKULIWA KWA HATUA KWA NIABA YA KIKUNDI.

Kwa kujisajili ili utumie akaunti kupitia mfumo wa paxful.com au tovuti zozote zinazohusiana, API au programu za vifaa vya mkononi, ikiwa ni pamoja na URL zozote zinazoendeshwa na Paxful (kwa ujumla “Tovuti ya Paxful” au “Tovuti”), unakubali kuwa umesoma kwa makini na kwa kina, kuelewa na kukubali vigezo na masharti yote yaliyo kwenye Makubaliano haya ikiwa ni pamoja na Sera yetu ya Faragha, Sera ya Vidakuzi na Idhini ya Sahihi ya Kielektroniki.

THAMANI YA MALI DIJITALI INAWEZA KUONGEZEKA AU KUPUNGUA NA PANAWEZA KUWA NA HATARI KUBWA KUWA UTAPOTEZA PESA KWA KUNUNUA, KUUZA, KUSHIKILIA AU KUWEKEZA KATIKA MALI DIJITALI. UNAPASWA KUZINGATIA KWA MAKINI IWAPO SHUGHULI YA KUFANYA BIASHARA AU KUSHIKILIA MALI DIJITALI INAKUFAA KULINGANA NA HALI YAKO YA KIFEDHA.

Kuhusu Paxful na Huduma zake

Paxful ni soko maarufu la mtu kwa mtu linalowezesha shughuli za ununuzi na uuzaji wa Mali Dijitali lenye wauzaji wanaokubali zaidi ya njia 300 za kulipa kwa kubadilishana na Mali zao Dijitali. Njia za kulipa hujadiliwa na kubadilishana kwa msingi wa mtu kwa mtu baina ya wanunuzi (“Wanunuzi”) na wauzaji (“Wauzaji”) walio Sokoni. Watumiaji wetu hukubaliana kuhusu njia za kulipa za kutumiwa ili kukamilisha shughuli ya ununuzi na uuzaji na wanawajibika kikamilifu kwa kutumia njia za kulipa kama hizo kwa njia ya kisheria.

Paxful pia hutoa huduma za pochi dijitali inayopangishwa kupitia mtoa huduma maarufu wa kimataifa wa pochi ya mali dijitali. Watumiaji wetu ulimwenguni kote wanaweza kuchapisha ofa za kununua au kuuza Mali Dijitali kwa njia mbalimbali rahisi. Mtoaji wa ofa anawajibika katika kuorodhesha vigezo vya shughuli za ununuzi na uuzaji, ikiwa ni pamoja na njia za kulipa ambazo Muuzaji atakubali. Baada ya ofa kuchaguliwa na mtumiaji mwingine wa Paxful, Mali Dijitali za Muuzaji hufungwa kama sehemu ya taratibu zetu za shughuli za ununuzi na uuzaji (tunazorejelea kama “Paxful Escrow”) hadi masharti yoyote yanayohitajika ili kukamilisha shughuli ya ununuzi na uuzaji yatimizwe. Shughuli ya uuzaji hukamilika na Mali Dijitali hufunguliwa na Muuzaji kuzipeana kwa Mnunuzi baada ya Mnunuzi kukamilisha vigezo vya shughuli ya ununuzi na uuzaji na malipo yamethibitishwa kuwa sahihi na kupokelewa na Muuzaji. PAXFUL HAIFANYI KAZI KAMA MCHAKATAJI WA MALIPO. DHIMA YOTE YA KUTUMA NA KUPOKEA MALIPO NA KUTHIBITISHA USAHIHI WA SHUGHULI ZA UNUNUZI NA UUZAJI IKO KATI YA MNUNUZI NA MUUZAJI. Mali Dijitali tunazofunga huachiliwa na kumilikiwa tena na Muuzaji ikiwa Mnunuzi ataamua kughairi shughuli ya ununuzi na uuzaji. Muuzaji hapaswi kughairi shughuli ya ununuzi na uuzaji wakati wowote. Muuzaji ana chaguo la kufungua tu Mali Dijitali na kuipeana kwa Mnunuzi. Hatua hii kwa ajili ya ulinzi wa usalama wa Mnunuzi. Iwapo Muuzaji atahitaji kughairi shughuli ya ununuzi na uuzaji kwa sababu ya Mnunuzi kutofuata vigezo vya shughuli ya ununuzi na uuzaji, ni lazima awasilishe ombi la mzozo na atoe sababu ya kufanya hivyo jinsi inavyobainishwa zaidi katika Sehemu ya 8 ya Makubaliano haya. Shughuli za mauziano kwenye Tovuti yetu hutekelezwa baina ya Wanunuzi na Wauzaji. Kwa hivyo, Paxful haihusiki kwenye muamala wowote.

Huduma inayopangishwa ya pochi ya sarafu dijitali inayotolewa na Paxful ni njia salama ya kuhifadhi, kutuma na kupokea sarafu dijitali. Paxful haihifadhi wala kushikilia Mali zozote Dijitali. Mali Dijitali huhifadhiwa kila wakati kwenye mitandao husika au kompyuta kadhaa ambazo zimeunganishwa kwenye mtandao wa mtu kwa mtu. Shughuli zote za ununuzi na uuzaji wa sarafu dijitali hufanyika ndani ya mtandao wa sarafu dijitali, wala si kwenye Paxful. Hakuna hakikisho lolote kuwa shughuli ya ununuzi na uuuzaji itachakatwa kwenye mtandao wa sarafu dijitali. Paxful inahifadhi haki ya kukataa kuchakata shughuli yoyote ya ununuzi na uuzaji ikiwa inahitajika kisheria au ikiwa tutachukuliwa kuwa shughuli hizo za ununuzi na uuzaji zinakiuka vigezo na masharti yetu yaliyo kwenye Makubaliano haya. Unakubali na kukiri kuwa unawajibika kikamilifu kwa shughuli zote zinazofanyika kwenye pochi yako na unakubali hatari zote za ufikiaji wowote wa pochi yako ulioidhinishwa au ambao haujaidhinishwa, kwa kiwango cha juu zaidi kinachoruhusiwa na sheria.

  1. MAELEZO YA JUMLA

    1. Tunahifadhi haki ya kurekebisha au kubadilisha Makubaliano haya wakati wowote, kwa hiari yetu sisi wenyewe na bila kutoa notisi ya mapema. Mabadiliko kama hayo yanayohusiana na matumizi yako ya Huduma yataanza kutumika yatakapochapishwa kwenye Tovuti ya Paxful na wala si kuanzia kipindi cha nyuma. Ikiwa umetupatia anwani yako ya barua pepe, tunaweza pia kukuarifu kupitia barua pepe kuwa Makubaliano yamerekebishwa. Ikiwa hukubaliani na vigezo vya Makubaliano yaliyorekebishwa, chaguo lako la pekee ni kukomesha matumizi yako ya Huduma na kufunga akaunti yako haraka iwezekanavyo.
    2. Ni wajibu wako kusoma Makubaliano haya kwa makini na kuyapitia mara kwa mara jinsi yalivyochapishwa kwenye Tovuti ya Paxful. Hatua yako ya kuendelea kutumia Huduma itamaanisha kuwa umekubali kufuata Makubaliano yatakayokuwa yanatumika kwa wakati huo.
    3. Hatua ya Paxful kuchelewa au kushindwa kutekeleza au kutotekeleza kikamilifu kifungu chochote cha Makubaliano haya, haipaswi kuchukuliwa kumaanisha kuwa tumesalimisha sheria au suluhu zetu zozote.
  2. AKAUNTI NA KUJISAJILI

    1. Ili uweze kutumia Huduma, utahitaji kufungua akaunti kupitia Tovuti yetu. Wakati wa mchakato wa kujisajili, tutakuomba utoe maelezo fulani, ikiwa ni pamoja na, wala si tu, jina lako, anwani na maelezo mengine ya kibinafsi ili kuthibitisha utambulisho wako. Tunaweza kwa hiari yetu sisi wenyewe kukataa kukufungulia akaunti. Unakubali na kukiri kuwa: (a) una umri unaokubalika kisheria na mamlaka ya mahali uliko ili kukubali Makubaliano haya; na (b) hujasimamishwa au kuondolewa kwenye matumizi ya Huduma zetu hapo awali.
    2. Kwa kutumia akaunti yako, unakubali na kuwakilisha kuwa utatumia Huduma zetu wewe mwenyewe na hutatumia akaunti yako kufanya shughuli za uajenti au uwakala kwa ajili ya kampuni, mtu au huluki nyingine yoyote. Isipokuwa uidhinishwe moja kwa moja na Paxful, unaruhusiwa kuwa na akaunti moja pekee na huruhusiwi kuuza, kukopa, kushiriki au kufanya akaunti yako ipatikane au maelezo yoyote yanayohitajika ili watu au huluki zingine kando na wewe ziweze kufikia akaunti yako. Unawajibika wewe mwenyewe katika kudumisha udhibiti na usalama wa kutosha kwa majina yoyote au yote ya mtumiaji, anwani za barua pepe, manenosiri, misimbo ya uthibitishaji wa hatua mbili au vitambulisho au misimbo mingine yoyote unayotumia kufikia Huduma. Akaunti yako haipaswi kuwa na maelezo ya kupotosha au ya uongo. Huruhusiwi kabisa kuweka maelezo ya uongo kwa akaunti yako, kudanganya kuhusu nchi yako ya asili au kutoa hati za uongo za vitambulisho.
    3. Wakati wa kufungua akaunti yako, unakubali kutupatia maelezo tunayoomba kwa madhumuni ya uthibitishaji wa utambulisho na utambuzi wa shughuli za ulanguzi wa fedha, ufadhili wa shughuli za kigaidi, utapeli au uhalifu mwingine wowote wa kifedha na kuturuhusu tuhifadhi rekodi ya maelezo kama hayo. Utahitaji kukamilisha taratibu fulani za uthibitishaji kabla ya kuruhusiwa kutumia Huduma, ambapo taratibu hizo zinaweza kubadilishwa kulingana na maelezo yanayokusanywa kukuhusu mara kwa mara. Maelezo tunayoomba yanaweza kujumuisha maelezo ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na, wala si tu, jina lako, anwani ya posta, namba ya simu, anwani ya barua pepe, tarehe ya kuzaliwa, namba ya ustawi wa jamii, namba ya kitambulisho cha mlipa ushuru na kitambulisho cha kitaifa. Kwa kutupatia maelezo hayo au maelezo mengine yoyote ambayo yanaweza kuhitajika, unathibitisha kuwa maelezo hayo yote ni ya kweli, sahihi na si ya kupotosha. Unakubali kutufahamisha haraka iwezekanavyo ikiwa maelezo yoyote uliyotupatia yatabadilika. UNATUPATIA IDHINI YA KUFANYA UDADISI, IWE KWA NJIA YA MOJA KWA MOJA AU KUPITIA WATU WENGINE, AMBAO TUNAZINGATIA KUWA UNAHITAJIKA ILI KUTHIBITISHA UTAMBULISHO WAKO AU KUKULINDA WEWE NA/AU KUJILINDA SISI WENYEWE DHIDI YA UTAPELI AU UHALIFU MWINGINE WA KIFEDHA, NA KUCHUKUA HATUA TUNAYOZINGATIA KUWA INAHITAJIKA KULINGANA NA MATOKEO YA UDADISI KAMA HUO. TUNAPOFANYA UDADISI HUO, UNAKUBALI NA KUKIRI KUWA MAELEZO YAKO YA KIBINAFSI YANAWEZA KUFICHULIWA KWA SHIRIKA LA UFUATILIAJI WA MIKOPO NA KUZUIA UTAPELI AU KWA MASHIRIKA YA KUSHUGHULIKIA UHALIFU WA KIFEDHA NA KUWA MASHIRIKA HAYO YANAWEZA KUSHUGHULIKIA UDADISI WETU KIKAMILIFU.
    4. Ikiwa unatumia Huduma kwa niaba ya huluki halali kama vile huluki ya kibiashara, unawakilisha na kuthibitisha zaidi kuwa: (i) huluki hiyo halali imeanzishwa ipasavyo na inahudumu kwa njia halali chini ya sheria zinazotumika za mamlaka ya uanzishaji wake; na (ii) umeidhinishwa ipasavyo na huluki halali kama hiyo ili kutenda kwa niaba yake. Akaunti ya kibiashara iliyothibitishwa ni mahususi kwa huluki hiyo halali na inaweza tu kutumiwa na mtu aliyeifungua. Akaunti za kibiashara haziruhusiwi kushirikiwa na au kutumiwa na watu au huluki zingine. Akaunti za kibiashara ambazo zimethibitishwa zimeruhusiwa kutumia hali chache zifuatazo za kipekee:

      • Akaunti ya kibiashara iliyoidhinishwa inaweza kuwa na akaunti kadhaa za watumiaji zinazotumika wakati wowote, mradi zote ziwe zimethibitishwa na kampuni na zinatumiwa na wafanyakazi waliotengwa wa kampuni ambao walifichuliwa na kuidhinishwa awali na Paxful kwa hiari yake yenyewe;
      • Akaunti za kibiashara zinapaswa kuwa ofa moja pekee inayotumika kwa shughuli mahususi ya ununuzi na uuzaji kwa wakati mmoja na haziruhusiwi kuwa na ofa nyingi kwa shughuli mahususi kama hiyo ya ununuzi na uuzaji kwenye akaunti zake nyingine za kibiashara.
    5. Unawajibika wewe mwenyewe kutengeneza nenosiri thabiti na kudumisha udhibiti na usalama wa kutosha kwa vitambulisho vyovyote au vyote, manenosiri, vidokezo, namba za utambulisho wa kibinafsi (PIN), funguo za API au misimbo mingine yoyote unayotumia kufikia Huduma zetu. Kupotea au kuathiriwa kwa maelezo yoyote yaliyotajwa na/au maelezo yako ya kibinafsi kunaweza kusababisha akaunti yako kufikiwa bila idhini na watu wengine na kupotea au kuibwa kwa Mali zozote Dijitali na/au fedha zinazohusishwa na akaunti yako, ikiwa ni pamoja na njia zako za kulipa zilizounganishwa na akaunti. Unawajibika wewe mwenyewe kusasisha anwani yako ya barua pepe, namba ya simu na maelezo mengine ya mawasiliano katika maelezo ya akaunti yako ili uweze kupokea arifa au notisi zozote ambazo tunaweza kukutumia. Hupaswi kamwe kuruhusu ufikiaji kwa mbali au kushiriki skrini ya kompyuta yako na mtu mwingine ukiwa umeingia katika akaunti yako. Hatuwajibiki kwa hasara yoyote ambayo unaweza kupata kwa sababu ya kuathiriwa kwa kitambulisho chako cha kuingia katika akaunti kwa sababu ya makosa yasiyo ya Paxful na/au kutofuata au kutochukua hatua kutokana na notisi au arifa tunazoweza kukutumia.
    6. Ili utumie Huduma zetu, unapaswa kutimiza majukumu fulani ya kisheria katika nchi yako na/au jimbo unakoishi. Kwa kukubali vigezo hivi vilivyo kwenye Makubaliano haya, unathibitisha kuwa umesoma kanuni na sheria za mahali uliko na kuwa unafahamu na unatimiza majukumu kama hayo yote. Kwa sababu ya vizuizi vya kisheria au vya kiusimamizi, hatutoi Huduma zetu katika maeneo fulani. Kwa kukubali vigezo vilivyo kwenye Makubaliano haya, unathibitisha kuwa wewe si mkazi au huongozwi na kanuni na sheria za maeneo hayo.
    7. Tunaweza kushindwa kufanya Huduma zote zipatikane kwenye masoko na maeneo yote na tunaweza kuzuia au kutokuruhusu matumizi ya sehemu au Huduma zote katika baadhi ya maeneo ("Maeneo yenye Vizuizi"). Kwa wakati huu maeneo yenye Vizuizi yanajumuisha nchi zile zilizo kwenye orodha yetu kama "(Orodha ya Nchi Zilizofungiwa)", na majimbo ya Washington na New York. Aidha, Huduma hazipatikani kulingana na sarafu ya kidijitali, Tether (USDT), kwa watumiaji wanaoishi Texas. Hupaswi kujaribu kutumia Huduma yetu ikiwa unaishi katika moja ya maeneo hayo Yaliyozuiliwa. Hupaswi kujaribu kuepuka kizuizi chochote kilichowekwa kupitia Huduma, kama vile kuhamisha anwani yako ya IP au kuwasilisha taarifa zozote zisizo sahihi kuhusu eneo lako.
  3. UTEKELEZAJI WA SHERIA, UPATANISHI NA UWEZO WA KUJITEGEMEA

    1. Makubaliano haya na matumizi yako ya Tovuti na Huduma yatasimamiwa na, na kufasiriwa kulingana na Jimbo la Delaware, bila kujali kanuni za utofauti wa sheria.
    2. Upatanishi. Wewe na Paxful mnakubaliana kuwa mzozo wowote unaotokana na au unaohusiana na Makubaliano haya au Huduma, hatimaye utasuluhishwa kwa upatanishi unaounganisha pande zote, kwa msingi wa mtu binafsi, kwa mujibu wa kanuni za Jumuiya ya Upatanishi ya Marekani za upatanishi wa mizozo inayohusiana na mtumiaji (zinazopatikana katika https://www.adr.org/rules). Kulingana na masharti ya utekelezaji wa sheria yanayotumika, walalamishi ambao ni watumiaji (watu ambao shughuli yao ya ununuzi na uuzaji imekusudiwa kwa matumizi ya kibinafsi, kifamilia au kinyumbani) wanaweza kuamua kuwasilisha madai yao katika mahakama ya eneo lao inayoshughulikia madai madogo kuliko kupitia upatanishi, mradi suala lao lisalie kwenye mahakama inayoshughulikia madai madogo na kushughulikiwa tu kwa msingi wa mtu binafsi (usio wa kikundi au usio wa uwakilishaji).

      USALIMISHAJI WA HAKI YA KUWASILISHA MADAI KWA NIABA YA KIKUNDI: KWA KIWANGO KINACHORUHUSIWA NA SHERIA, MADAI YOTE YATAWASILISHWA KWA MSINGI WA MTU BINAFSI WALA SI KAMA MDAI AU MWANACHAMA WA KIKUNDI KWENYE KIKUNDI CHOCHOTE KINACHODAIWA, HATUA YA JUMLA AU KESI YA UWAKILISHAJI (KWA UJUMLA “USALIMISHAJI WA HAKI YA KUWASILISHA MADAI KWA NIABA YA KIKUNDI”). MPATANISHI HAPASWI KUJUMUISHA MADAI ZAIDI YA MOJA YA MTU AU KUJIHUSISHA KWENYE UPATANISHI WOWOTE WA KIKUNDI. UNAKIRI KUWA, KWA KUKUBALI VIGEZO HIVI, WEWE NA PAXFUL MNASALIMISHA HAKI YOYOTE YA KUAMULIWA KWA MZOZO WENU NA HAKIMU NA MNASALIMISHA HAKI YA KUSHIRIKI KATIKA UWASILISHAJI WA MADAI KWA NIABA YA KIKUNDI DHIDI YA PAXFUL.

      Sheria ya Upatanishi ya Nchi, 9 U.S.C. §§ 1-16, inatumika kikamilifu katika upatanishi. Upatanishi utatekelezwa na mpatanishi mmoja asiyeegemea upande wowote na utafanyika katika Jimbo la Delaware au eneo tofauti litakalokubaliwa na pande zote, kwa lugha ya Kiingereza. Mpatanishi anaweza kutoa fidia ambayo mahakama ya uwezo thabiti wa kutekeleza sheria inaweza kutoa, ikiwa ni pamoja na ada za wakili akiidhinishwa na sheria, na uamuzi wa upatanishi utarekodiwa kama hukumu na kutekelezwa katika mahakama yoyote ya kisheria. Kwa ombi lako, kesi zinaweza kusikilizwa kwa njia ya kuhudhuria moja kwa moja au kupitia simu na mpatanishi anaweza kuruhusu mijadala ya uwasilishaji wa madai na uamuzi wa kesi kwa maelezo mafupi, bila upande wowote kuhudhuria kesi. Mhusika atakayeshinda katika uamuzi au kesi yoyote ya kutekelezwa kwa Makubaliano haya atakuwa na haki ya kufidiwa pesa alizotumia na ada za wakili.

      Ikiwa mpatanishi/wapatanishi au msimamizi wa upatanishi atakutoza ada za kuwasilisha kesi au gharama nyingine za usimamizi, tutakufidia, utakapotuma maombi, kwa kiwango ambacho ada au gharama hizo zitazidi ada au gharama ambazo huenda ungepaswa kulipa ikiwa kesi yako ingekuwa inashughulikiwa mahakamani badala yake. Tutalipa pia ada au gharama za ziada ikiwa tutahitajika kufanya hivyo kulingana na kanuni za msimamizi wa upatanishi au sheria inayotumika. Kando na hayo, kila mhusika atawajibika kwa ada au gharama nyingine zozote, kama vile ada za wakili ambazo mhusika anaweza kutozwa.

    3. Ikiwa sehemu yoyote ya Makubaliano haya itazingatiwa kuwa haitumiki au haiwezi kutekelezwa kikamilifu au kwa sehemu yake na mpatanishi au mahakama yoyote ya Marekani, uwezo wa kutumika au kutekelezwa kwa vifungu vingine vya vigezo na masharti haya hautaathirika. Vichwa vyovyote vilivyo kwenye Makubaliano haya vimekusudiwa kwa madhumuni ya kutoa maelezo pekee na si vifungu vinavyoweza kutekelezwa vya Makubaliano haya.
  4. SERA YA FARAGHA NA USALAMA

    1. Tunaahidi kuchukua hatua zote zinazofaa ili kulinda maelezo yako ya kibinafsi. Hata hivyo, hatuwezi kukuhakikishia usalama wa data yoyote unayofichua mtandaoni. Unakubali hatari zinazohusiana na kutoa maelezo na kufanya shughuli zako mtandaoni na hutatuwajibisha kwa hali yoyote ya ukiukaji wa usalama isipokuwa hali hiyo iwe inatokana na utepetevu wetu.
    2. Tafadhali soma taarifa yetu rasmi ya faragha: https://paxful.com/privacy.
  5. HAKUNA DHAMANA, KIMA CHA WAJIBU & KUKUBALI HATARI

    1. HUDUMA ZINATOLEWA KWA MSINGI WA “JINSI ZILIVYO” NA “JINSI ZINAVYOPATIKANA” BILA DHAMANA, UWAKILISHAJI AU HAKIKISHO ZOZOTE, IWE NI KWA NJIA YA MOJA KWA MOJA, INAYODHANIWA AU YA KISHERIA. KWA KIWANGO CHA JUU ZAIDI KINACHORUSIWA NA SHERIA INAYOTUMIKA, PAXFUL INAPINGA KWA NJIA MAHUSUSI DHAMANA ZOZOTE ZINAZODHANIWA ZA JINA, UBORA UNAOKUBALIKA KIBIASHARA, UFAAFU KWA MADHUMUNI FULANI NA/AU KUTOKIUKWA KWA HAKI. PAXFUL HATOI UWAKILISHAJI AU DHAMANA ZOZOTE KUWA TOVUTI, SEHEMU YOYOTE YA HUDUMA AU NYENZO ZOZOTE ZILIZO HAPA, ZITAPATIKANA KILA WAKATI, BILA KUKATIZWA, KWA WAKATI AU BILA HITILAFU YOYOTE. PAXFUL HAIWAJIBIKI KWA UKATIZWAJI WA HUDUMA AU HASARA YOYOTE AMBAYO MTUMIAJI ANAWEZA KUPATA. UNAKIRI NA KUKUBALI KUWA UMESOMA NA KUELEWA TAARIFA HII NA WALA SI TAARIFA NYINGINE YOYOTE, IWE KWA MAANDISHI AU KWA KUTAMKWA, KUHUSIANA NA MATUMIZI NA UFIKIAJI WAKO WA HUDUMA NA TOVUTI. KANDO NA YALIYOTAJWA, UNAKIRI NA KUKUBALI HATARI MBALIMBALI ZINAZOHUSIANA NA MATUMIZI YA SARAFU DIJITALI, IKIWA NI PAMOJA NA, WALA SI TU, KIFAA KUACHA KUFANYA KAZI, MATATIZO YA PROGRAMU, KUSHINDWA KUUNGANISHA KWENYE MTANDAO, PROGRAMU HASIDI, UINGILIAJI KATI WA WATU WENGINE UNAOSABABISHA HASARA AU KUTOWEZA KUFIKIA AKAUNTI AU POCHI YAKO NA DATA NYINGINE YA MTUMIAJI, MATATIZO YA SEVA AU KUPOTEA KWA DATA. UNAKUBALI NA KUKIRI KUWA PAXFUL HAITAWAJIBIKA KWA HALI ZOZOTE ZA MATATIZO YA MAWASILIANO, KUKATIZWA KWA MAWASILIANO, HITILAFU ZA MAWASILIANO, KUATHIRIWA KWA MAWASILIANO AU KUCHELEWESHWA KWA MAWASILIANO, AMBAZO UNAWEZA KUKUMBANA NAZO UNAPOTUMIA HUDUMA, BILA KUJALI VYANZO VYAKE.
    2. PAXFUL, WASHIRIKA NA WATOA HUDUMA WAKE, AU MAOFISA, WAKURUGENZI, MAWAKALA, WAFANYAKAZI, WASHAURI AU WAWAKILISHI WAKE HUSIKA, HAWATAWAJIBIKA KWA NAMNA YOYOTE KWA (A) KIASI CHOCHOTE CHA PESA KINACHOZIDI THAMANI YA JUMLA YA ADA UNAYOPASWA KULIPA KWA HUDUMA HUSIKA KATIKA KIPINDI CHA MIEZI KUMI NA MBILI (12) KABLA YA KUTOKEA KWA HASARA (B) KWA FAIDA YOYOTE ULIYOPOTEZA, KUPUNGUA THAMANI AU FURSA YA BIASHARA, HASARA, UHARIBIFU, UFISADI AU UVUJAJI WA DATA AU MALI NYINGINE YOYOTE ISIYOSHIKIKA AU UHARIBIFU WOWOTE MAALUM, WA BAHATI MBAYA, USIO WA MOJA KWA MOJA, USIOSHIKIKA, AU UNAOTOKANA NA MATUMIZI, IWE NI KULINGANA NA MKATABA, UKIUKAJI WA HAKI, UTEPETEVU, DHIMA KALI, AU UNAOTOKANA NA AU KUHUSIANA NA MATUMIZI YALIYOIDHINISHWA AU YASIYOIDHINISHWA YA TOVUTI AU HUDUMA, AU MAKUBALIANO HAYA, HATA KAMA MWAKILISHI WA PAXFUL ALIYEIDHINISHWA AMESHAURIWA AU ALIJUA AU ALIPASWA KUJUA UWEZEKANO WA KUTOKEA KWA UHARIBIFU KAMA HUO, NA LICHA YA KUSHINDWA KUTIMIZA MADHUMUNI AU KUTOA SULUHU NYINGINE MUHIMU ILIYOKUBALIWA, ISIPOKUWA KWA KIWANGO CHA HUKUMU YA MWISHO YA MAHAKAMA KUWA UHARIBIFU KAMA HUO ULITOKANA NA UTEPETEVU MKUBWA WA PAXFUL, UDANGANYIFU, UKIUKAJI WA MAADILI AU UKIUKAJI WA SHERIA KIMAKUSUDI. BAADHI YA MAMLAKA HAZIRUHUSU KUTENGWA AU KUTOJUMUISHWA KWA UHARIBIFU WA BAHATI MBAYA AU UNAOTOKANA NA MATUMIZI, KWA HIVYO HUENDA KIKOMO CHA HAPO JUU HAKITATUMIKA KWAKO.
    3. Hatumiliki wala kudhibiti itifaki zinazotumika za programu ambazo zinazosimamia utendakazi wa Mali Dijitali. Kwa kawaida, itifaki zinazotumika ni za programu huria na mtu yeyote anaweza kuzitumia, kuzinakili, kuzibadilisha na kuzisambaza. Hatuwajibiki kwa utendakazi wa itifaki zinazotumika na hatuwezi kuhakikisha utendakazi au usalama wa shughuli za mtandao. Hasa, itifaki zinazotumika zinaweza kutegemea mabadiliko ya ghafla ya kanuni za utendakazi (ikiwa ni pamoja na “mageuzi”). Mabadiliko makubwa kama hayo ya utendakazi yanaweza kuathiri kwa kiwango kikubwa upatikanaji, thamani, utendakazi na/au jina la sarafu dijitali. Paxful haidhibiti vipengele na wakati wa kufanywa kwa mabadiliko makubwa kama hayo ya utendakazi. Ni wajibu wako kujifahamisha kuhusu mabadiliko ya utendakazi yajayo na unapaswa kuzingatia kwa makini maelezo yanayopatikana hadharani na maelezo yanayoweza kutolewa na Paxful ili kubaini ikiwa utaendelea kutumia Huduma. Mabadiliko ya utendakazi kama hayo yanapotokea, Paxful inahifadhi haki ya kuchukua hatua jinsi ambavyo huenda inahitajika ili kulinda usalama na utendakazi salama wa mfumo wake, ikiwa ni pamoja na kusimamisha kwa muda utendakazi wa sarafu dijitali inayohusika/zinazohusika na kuchukua hatua nyingine zinazohitajika. Paxful itatumia juhudi zake zinazofaa ili kukupa notisi ya jinsi inavyoshughulikia mabadiliko yoyote makubwa ya utendakazi; hata hivyo, hatuna uwezo wa kudhibiti mabadiliko kama hayo na yanaweza kutendeka bila kutoa notisi kwa Paxful. Jinsi tunavyoshughulikia mabadiliko yoyote makubwa ya utendakazi inategemea hiari yetu sisi wenyewe na ni pamoja na kuamua kutotumia mageuzi yoyote mapya au vitendo vingine. Unakiri na kukubali hatari za mabadiliko ya utendakazi kwa itifaki za Mali Dijitali na unakubali kuwa Paxful haiwajibiki kwa mabadiliko kama hayo ya utendakazi na haiwajibiki kwa hasara yoyote ya thamani unayoweza kupata kwa sababu ya mabadiliko kama hayo ya kanuni za utendakazi. Unakiri na kukubali kuwa Paxful inaweza kuamua kushughulikia mabadiliko yoyote ya utendakazi kwa hiari yake yenyewe na kuwa hatuna wajibu wowote wa kukusaidia kutumia sarafu au itifaki zisizotumika.
    4. Kwa kutumia Huduma zetu, unaweza kuangalia maudhui au kutumia Huduma zinazotolewa na watu wengine, ikiwa ni pamoja na viungo vya kuelekeza kwa tovuti na huduma za watu wengine kama hao (“Maudhuiya watu wengine”). Hatuidhinishi, kuiga au kudhibiti maudhui yoyote ya watu wengine na hatutawajibika au kuwa dhima ya namna yoyote kwa maudhui ya watu wengine kama hayo. Zaidi ya hayo, shughuli au mawasiliano yako na watu wengine kama hao ni baina yako na watu hao wengine. Hatuwajibiki kwa hasara au uharibifu wa namna yoyote utakaopatikana kutokana na shughuli zozote kama hizo na unaelewa kuwa mawasiliano na matumizi yako ya maudhui ya watu wengine ni kwa tahadhari yako wewe mwenyewe.
    5. Kwa ajili ya kuondoa shaka, Paxful haitoi ushauri wa uwekezaji, ushuru au wa kisheria. Paxful haijasajiliwa na Tume ya Marekani ya Ubadilishaji wa Hisa na Amana na haitoi huduma za amana au ushauri wa uwekezaji. Shughuli zote za ununuzi na uuzaji kupitia Soko letu hufanyika kwa msingi wa mtu kwa mtu baina ya Muuzaji na Mnunuzi na unawajibika wewe mwenyewe katika kubaini ikiwa uwekezaji, mikakati ya uwekezaji au shughuli yoyote husika ya ununuzi na uuzaji inakufaa kulingana na malengo yako ya kibinafsi ya uwekezaji, hali za kifedha na uvumiliaji wa hatari. Unapaswa kushauriana na mtaalamu wako wa masuala ya kisheria au ushuru kuhusiana na hali yako mahususi. Mara kwa mara, tunaweza kutoa maelezo ya kielimu kuhusu bidhaa na mfumo wetu, ili kusaidia watumiaji wapate maelezo zaidi kuhusu Huduma zetu. Maelezo yanaweza kuwa ni pamoja na, wala si tu, machapisho ya blogu, makala, viungo vya kuelekeza kwa maudhui ya watu wengine, mipasho ya habari, mafunzo na video. Maelezo yanatolewa kwenye Tovuti au kwenye tovuti zozote za watu wengine si ushauri wa uwekezaji, kifedha, kibiashara au ushauri wa namna nyingine yoyote, na hupaswi kuchukulia maudhui yoyote ya Tovuti kama ushauri wa namna yoyote. Kabla ya kuamua kununua, kuuza au kushikilia Mali yoyote Dijitali, unapaswa kufanya uchunguzi wako mwenyewe wa kina na kuwasiliana na washauri wako wa masuala ya kifedha kabla ya kufanya uamuzi wowote wa uwekezaji. Paxful haitawajibika kwa maamuzi utakayofanya ya ununuzi, uuzaji au ushikiliaji wa Mali Dijitali kulingana na maelezo yanayotolewa na Paxful.
    6. Unakubali kuwa hatuwajibiki kwa mabadiliko yoyote ya bei ya Mali Dijitali. Iwapo hali yoyote ya kutatiza shughuli za kawaida za sokoni itatokea au tukio Lisiloweza Kuepukika (jinsi ilivyobainishwa kwenye Kifungu cha 17), tunaweza kufanya mojawapo au zaidi ya mambo yafuatayo: (a) kusimamisha ufikiaji wa Huduma; au (b) kukuzuia kufanya vitendo vyovyote kupitia Huduma. Hatutawajibika kwa hasara zozote utakazopata kutokana na vitendo kama hivyo. Kufuatia tukio kama hilo, Huduma zitakapoanza kutumika tena, unakiri kuwa bei zitakazokuwa zinatumika sokoni zinaweza kutofautiana kwa kiwango kikubwa na bei zilizokuwa zikitumika kabla ya tukio kama hilo kutokea.
    7. Hatutoi hakikisho lolote kuwa Tovuti au seva inayoiendesha haina virusi au hitilafu zozote, kuwa maudhui yake ni sahihi, kuwa huduma yake haitakatizwa au kuwa hitilafu zitarekebishwa. Hatutawajibika kwako kwa hasara ya namna yoyote utakayopata, kutokana na kitendo unachofanya au ulichofanya kwa kutegemea nyenzo au maelezo yaliyo kwenye Tovuti.
  6. KUTOA MSAMAHA KWA PAXFUL NA FIDIA

    1. Ikiwa kuna mzozo baina yako na mtumiaji mmoja au zaidi wa Huduma zetu, iwapo utatoa msamaha kwa Paxful, washirika na watoa huduma wake na kila mmoja wa maofisa, wakurugenzi, wafanyakazi, maejenti na wawakilishi wake, kutokana na madai yoyote au yote, matakwa au uharibifu (uharibifu halisi na unaotokana na matumizi) wa aina na hali yoyote unaotokana na au unaohusiana kwa namna yoyote na mizozo kama hiyo. Unakubali kufidia na kutowajibisha Paxful, washirika wake na kila mmoja wa maofisa, wakurugenzi, wafanyakazi, maejenti na wawakilishi wake kwa madai au matakwa yoyote (ikiwa ni pamoja na ada za wakili na faini zozote, ada au adhabu zilizotolewa na mamlaka yoyote ya usimamizi) yanayotokana na au yanayohusiana na ukiukaji wako wa Makubaliano haya au ukiukaji wako wa sheria, kanuni au haki zozote za mtu mwingine
  7. SHUGHULI ZA UNUNUZI NA UUZAJI KWENYE SOKO LA PAXFUL

    Tovuti inawaruhusu watumiaji kuomba ofa za kununua na kuuza Mali Dijitali.

    Mtumiaji anapoanzisha shughuli ya ununuzi na uuzaji wa Mali Dijitali, shughuli hiyo ya ununuzi na uuzaji hukamilishwa kwa mujibu wa Makubaliano haya na vigezo vya ziada, iwapo vipo, vilivyobainishwa na mtumiaji au mhusika mwingine anayeshiriki katika shughuli hiyo. Mwongozo wa hatua kwa hatua kuhusu ununuzi na uuzaji wa Mali Dijitali kwenye Soko la Paxful unapatikana katika https://support.paxful.com/support/solutions/150000191612.

    Vigezo vya jumla vifuatavyo vinatumika kwa kila shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyobainishwa hapa chini:

    1. Kununua Mali Dijitali kupitia uombaji wa ofa.

      Unaponunua Mali Dijitali kwenye Soko la Paxful:

      1. Hakuna ada zozote za Eskro ya Paxful kama sehemu ya shughuli ya ununuzi na uuzaji ambazo zinapaswa kulipwa na Wanunuzi kwenye Soko letu.
      2. Ofa kutoka kwa wahusika wengine wanaoshiriki katika shughuli ya ununuzi na uuzaji kwenye Paxful zina vigezo na masharti yake na kila ofa itatofautiana katika bei ya ubadilishanaji, kasi ya ubadilishanaji na vigezo na masharti mengine yaliyowekwa na Muuzaji. Kwa kukubali ofa ya Muuzaji, unakubali kufuata vigezo na masharti ya ofa hiyo. Vigezo na masharti yaliyobainishwa na Muuzaji hutumika kwa hali zote isipokuwa iwapo yanatofautiana au yanakiuka Makubaliano haya, si halali, hayafai au ni magumu kuyafuata (jinsi inavyobainishwa na Paxful kwa hiari yake yenyewe), au ikiwa watumiaji wote wawili wanaoshiriki katika shughuli ya ununuzi na uuzaji watakubali kurekebisha vigezo na masharti ya ofa kama hiyo. NI WAJIBU WAKO KUSOMA KWA MAKINI VIGEZO NA MASHARTI YA OFA YA MUUZAJI NA KUYAFUATA JINSI YALIVYO. IKIWA HUTAFUATA VIGEZO NA MASHARTI YA OFA, MALIPO YAKO HAYATAKUBALIWA. USIWAHI KAMWE KUTUMA MALIPO ISIPOKUWA UWE UMEFUATA VIGEZO NA MASHARTI YOTE YALIYOORODHESHWA KWENYE OFA. UKITUMA MALIPO BILA KUFUATA VIGEZO NA MASHARTI, PAXFUL HAIWEZI KUKUSAIDIA KATIKA MCHAKATO WA MZOZO WA KUREJESHA MALIPO YAKO.
      3. Uthibitishaji wa malipo na utoaji wa maagizo ya kufungua Mali Dijitali kwenye Eskro ya Paxful ni majukumu ya Muuzaji pekee wala si ya Paxful. Ikiwa Muuzaji hataachilia Mali Dijitali kwako baada ya kukamilisha vigezo na masharti ya Muuzaji ipasavyo, ripoti suala hilo haraka iwezekanavyo kupitia kitufe cha kuwasilisha mizozo kilichotengwa kinachopatikana katika sehemu ya kupiga gumzo ya shughuli husika ya ununuzi na uuzaji. Huduma kwa wateja ya Paxful itakagua na kusuluhisha mzozo huo. Mchakato huu wa usuluhishaji wa mizozo umeelezewa zaidi hapa chini katika “Kifungu cha 8 - Kuwasilisha Mizozo ya Shughuli ya Ununuzi na Uuzaji Kupitia Mchakato wa Usuluhishaji wa Mizozo wa Paxful.” Ikiwa hutafuata mchakato huu wa usuluhishaji wa mizozo, Paxful haitaweza kukusaidia kwa suala hilo.
    2. Uuzaji wa Mali Dijitali

      Unapouza Mali Dijitali kwenye Soko la Paxful:

      1. Ni lazima Wauzaji wathibitishe na kuchakata malipo kwa wakati unaofaa na ndani ya kipindi fulani cha muda jinsi ilivyobainishwa kwenye vigezo vya ofa. Baada ya Mnunuzi kukutumia malipo kulingana na vigezo vya ofa, ni wajibu na jukumu lako kuthibitisha na kuchakata malipo haraka iwezekanavyo na kisha ufungue Mali Dijitali kwenye Eskro ya Paxful na kuiachilia kwa Mnunuzi. Ikiwa hutafuata maagizo yaliyo kwenye ofa, hutakuwa na haki ya kurejeshewa Mali zako Dijitali.
      2. Kama Muuzaji, unakubali hatari na dhima zote za ukiukaji wa Makubaliano haya utakazopata kupitia uuzaji wa Mali Dijitali. Ni wajibu wako kulipa ushuru wote unaopaswa kulipwa. Paxful itakutoza ada fulani kama Muuzaji wa Mali Dijitali kwa kufunga Mali Dijitali kwenye Eskro ya Paxful kabla ya uuzaji. Isipokuwa ibainishwe vinginevyo na Paxful kwa hiari yake yenyewe, Paxful haitafidia hasara zozote ambazo Muuzaji atapata iwe zinatokana na ukiukaji wa Makubaliano haya, udanganyifu au vinginevyo na hatutarejesha ada yetu tunayotoza kwa hali zozote.
      3. Malipo yoyote yanayopokelewa yanapaswa kuchakatwa kikamilifu na kuthibitishwa kuwa umeyapokea kabla ya kufungua Mali Dijitali kwenye Eskro ya Paxful. Paxful haiwajibiki kwa hasara utakayopata ikiwa utafungua Mali Dijitali mapema kabla hujapokea na kuthibitisha malipo. Ni lazima uwe msikivu na umjibu Mnunuzi wako. Unapaswa kutowezesha ofa zozote ambazo hazitumiki.
      4. Utangazaji wowote wa tovuti yako mwenyewe katika sehemu yoyote ya Soko la Paxful (kama vile wasifu wako, vigezo vya ofa au gumzo ya shughuli ya ununuzi na uuzaji) ambao utawezesha ununuzi na uuzaji wa Mali Dijitali nje ya Huduma za Paxful hauruhusiwi kabisa. Katika hali chache, unaruhusiwa kushiriki tovuti yako ambayo umetengeneza kwa madhumumi ya Muuzaji kupokea malipo pekee ili kukamilisha shughuli ya ununuzi na uuzaji (yaani, uchakataji unaoaminika wa kadi ya mikopo/benki wa mtu mwingine) kwenye maagizo ya shughuli ya ununuzi na uuzaji; muradi matumizi ya tovuti za nje kama hizo yamebainishwa kwenye vigezo vya ofa na tovuti kama hizo hazipaswi kuwa na matangazo mengine yoyote au maelezo yako ya mawasiliano.
    3. Utiifu

      1. Paxful na Huduma hazishirikishwi au kuhusishwa na, wala kuidhinishwa au kufadhiliwa na mtu mwingine yeyote, ikiwa ni pamoja na, wala si tu mtoaji yeyote wa kadi. Alama za biashara, chapa na vitambulishi vingine vilivyotengwa ni mali ya wamiliki wake husika pekee. Paxful na Huduma zake haziidhinishwi, kufadhiliwa, kuhusishwa au kushirikishwa kwa njia yoyote na au wamiliki kama hao.
      2. Paxful si muuzaji wa kadi za zawadi aliye na leseni au muuzaji aliyeidhinishwa wa mtoaji yeyote wa kadi za zawadi. Kadi zozote za zawadi unazopkea moja kwa moja kutoka kwa mtumiaji anayetumia Soko la Paxful zinategemea vigezo na masharti ya muuzaji mwingine ambako inaweza kukombolewa (“Mtoaji”). Paxful haiwajibiki kwa vitendo au kwa kutojumuishwa kwa Mtoaji/Watoaji wowote au ada zozote, tarehe za mwisho wa matumizi, adhabu au vigezo na masharti yanayohusishwa na kadi ya zawadi ya Mtoaji iliyopokelewa kupitia Soko la Paxful. Kwa kupokea kadi ya zawadi kutoka kwa mtumiaji, unakubali kuwa umesoma vigezo na masharti ya kadi hiyo ya zawadi, na unawakilishi kwa Paxful kuwa unastahiki kutumia kadi za zawadi kama hizo chini ya vigezo na masharti ya Mtoaji wa kadi hiyo ya zawadi, au chini ya sheria inayotumika.
      3. KUFANYA UDALALI AU UUZAJI WA KADI ZA ZAWADI HAURUHUSIWI KABISA KWENYE TOVUTI NA SOKO LETU. NI LAZIMA UWE MMILIKI KAMILI WA KADI YA ZAWADI, NA KWA OMBI LA PAXFUL, UNAKUBALI KUTOA UTHIBITISHO SAHIHI WA UMILIKI WA KADI YAKO YA ZAWADI KWA PAXFUL (KAMA VILE RISITI). PAXFUL HAITOI MADAI, UWAKILISHAJI AU HAKIKISHO LOLOTE KUWA NJIA ZOZOTE ZA KULIPA ZA MTU MWINGINE ZILIZO KWENYE TOVUTI ZINARUHUSU KUFANYWA KWA SHUGHULI YA UNUNUZI NA UUZAJI KUPITIA HUDUMA YA PAXFUL, AU KUWA NJIA ZOZOTE ZA KULIPA ZA MTU MWINGINE ZILIZO KWENYE TOVUTI YETU ZINARUHUSU AU ZINARUHUSIWA NA HUDUMA ZETU. HUPASWI KUTUMIA NJIA ZA KULIPA ZA MTU MWINGINE KAMA HIZO KWENYE PAXFUL IKIWA MTU MWINGINE KAMA HUYO HARUHUSU MATUMIZI YAKE
      4. UNAWAJIBIKA KIKAMILIFU KATIKA KUFUATA KANUNI NA SHERIA ZOTE ZINAZOTUMIKA KATIKA ENEO LA MAMLAKA AMBAKO SHUGHULI YAKO YA UNUNUZI NA UUZAJI INAFANYIKA.
      5. Ni lazima shughuli zote za ununuzi na uuzaji zifanyiwe kwenye Paxful. Kufanyia shughuli za ununuzi na uuzaji nje ya mfumo wa Paxful au ubadilishanaji wa anwani za mawasiliano za nje hauruhusiwi kabisa.
    4. Vikomo vya Uhamishaji. Tunaweza kwa hiari yetu sisi wenyewe kuweka vikomo au vikwazo kwa ukubwa, aina au namna ya shughuli zozote za uhamishaji zinazopendekezwa, kama vile kuweka kikomo kwa kiasi cha jumla cha Mali Dijitali zinazoweza kuchapishwa kwa ajili ya kuuzwa.
    5. Hakuna Hakikisho. Paxful haitoi hakikisho kuwa utaweza kuuza Mali Dijitali kwenye Soko lake. Kitendo cha kununua au kuuza Mali Dijitali kupitia Soko la Paxful si hakikisho kuwa utaweza kununua au kuuza Mali Dijitali kupitia Soko hilo kila wakati.
    6. Uhusiano. Hakuna chochote kwenye Makubaliano haya kinachokusudiwa kwa au kitakachounda ushirika, biashara ya pamoja, shirika, huduma ya ushauri au uamana wowote, ikizingatiwa kuwa wewe na Paxful ni wakandarasi wanaojitegemea.
    7. Usahihi wa Maelezo. Unawakilisha na kutoa dhamana kuwa maelezo yoyote unayotoa kupitia Huduma ni sahihi na kamili. Unakubali na kukiri kuwa Paxful haiwajibiki kwa makosa yoyote unayofanya ya hitilafu au kutojumuishwa kwa maelezo yoyote yanayohusiana na shughuli yoyote ya ununuzi na uuzaji inayoanzishwa kupitia Huduma, kwa mfano, ukiandika anwani ya Pochi visivyo au vinginevyo utoe maelezo yasiyo sahihi. Tunakuhimiza zaidi ukague maelezo yako ya shughuli ya ununuzi na uuzaji kwa makini kabla ya kuyachapisha kupitia Huduma.
    8. Hakuna Kughairi au Kufanya Mabadiliko; Shughuli za Pochi. Baada ya maelezo ya shughuli ya ununuzi na uuzaji kutumwa kwenye mtandao wa sarafu dijitali kupitia Huduma, Paxful haiwezi kukusaidia kughairi au kubadilisha shughuli yako ya ununuzi na uuzaji. Paxful haina uwezo wa kudhibiti mtandao wowote wa sarafu dijitali na haina uwezo wa kuwezesha maombi yoyote ya kughairi au kufanya mabadiliko. Paxful haihifadhi wala kushikilia Mali zozote Dijitali zilizofungwa. Mali Dijitali hurekodi kwenye mitandao au mitandao yake husika ya kurekodi maelezo kila wakati. Shughuli zote za ununuzi na uuzaji wa sarafu dijitali hufanyika ndani ya mtandao wa sarafu dijitali wala si kwenye Paxful. Hakuna hakikisho zozote kuwa shughuli ya ununuzi na uuzaji itachakatwa kwenye mtandao wa sarafu dijitali. Paxful inahifadhi haki ya kukataa kuchakata shughuli yoyote ya ununuzi na uuzaji ikiwa inahitajika kisheria au ikiwa tutachukulia kuwa shughuli hizo za ununuzi na uuzaji zinakiuka vigezo na masharti yetu yaliyo kwenye Makubaliano haya. Unakubali na kukiri kuwa unawajibika kikamilifu kwa shughuli zote zinazofanyika kwenye Pochi yako na unakubali hatari zote za ufikiaji ulioidhinishwa au ambao haujaidhinishwa kwa pochi yako, kwa kiwango cha juu zaidi kinachoruhusiwa na sheria.
    9. Ushuru. Ni wajibu wako kubaini ni ushuru gani, iwapo upo, unaotumika kwa shughuli za ununuzi na uuzaji ambazo umetuma maelezo yake kupitia Huduma, na ni wajibu wako kuripoti na kulipa ushuru sahihi kwa mamlaka inayofaa. Unakubali kuwa Paxful haiwajibiki katika kubaini ikiwa ushuru unatumika kwa shughuli zako za ununuzi na uuzaji wa sarafu dijitali au kwa kukusanya, kuripoti, kuzuia au kulipa ushuru wowote unaotokana na shughuli zozote za ununuzi na uuzaji wa sarafu dijitali.
    10. Sifa za Mtumiaji. Unapojihusisha kwenye Shughuli ya Ununuzi na Uuzaji, tunaruhusu watumiaji wengine kutoa maoni kuhusu jinsi walivyoshirikiana nawe. Tunaruhusu pia watumiaji kuwasilisha ripoti ikiwa wanaamini kuwa umekiuka Makubaliano haya kwa njia yoyote. Ripoti hizi ni za siri, lakini tunaweza kuzitumia kuhusiana na mzozo fulani jinsi ilivyobainishwa katika Kifungu cha 8.
    11. Historia ya Shughuli ya Ununuzi na Uuzaji. Unaweza kuangalia historia ya shughuli yako ya ununuzi na uuzaji kupitia Akaunti yako. Unakubali kuwa hali ya Huduma kushindwa kutoa maelezo kama hayo haitahujumu au kufanya vigezo vya shughuli ya ununuzi na uuzaji kama hiyo kutotumika.
    12. Paxful Pay. Paxful imeidhinisha wauzaji fulani kukubali Paxful kama njia ya kulipia ununuzi wa bidhaa na huduma mtandaoni (“Wauzaji Walioidhinishwa”). Unaweza kulipa Muuzaji Aliyeidhinishwa kwa kuteua chaguo la “Paxful Pay” unapoondoka au wakati wa kulipa. Chaguo la Paxful Pay litakuelekeza kwa Soko letu ili ufikie Mali Dijitali zinazopatikana kwenye akaunti yako au kukuunganisha kwa Muuzaji. Ukinunua Mali Dijitali kutoka kwa Muuzaji ili ukamilishe shughuli ya ununuzi na uuzaji, vigezo vilivyobainishwa katika Kifungu cha 7.1 cha Makubaliano haya vitatumika.
    13. Bidhaa za Muuzaji. Paxful haiwajibiki kwa bidhaa au huduma zozote unazoweza kununua kutoka kwa Muuzaji Aliyeidhinishwa kwa kutumia akaunti yako au bidhaa ya Paxful Pay. Ikiwa una mzozo na Muuzaji yeyote Aliyeidhinishwa, unapaswa kusuluhisha mzozo huo moja kwa moja na Muuzaji huyo Aliyeidhinishwa.
    14. Urejeshaji wa Bidhaa au Pesa. Unaponunua bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mwingine kwa kutumia Akaunti yako, huwezi kutendua shughuli hiyo. Hatushughulikii masuala ya urejeshaji wa bidhaa au pesa. Muuzaji Aliyeidhinishwa anaweza kukurejeshea pesa, punguzo la bidhaa dukani au kadi ya zawadi kwa hiari yake mwenyewe na kwa mujibu wa sera zake.
    15. Paxful hutoza ada za Huduma, ada zinazotumika zitaonyeshwa mapema kabla hujatumia Huduma yoyote ambayo inatozwa ada. Angalia “Ada za Paxful” kwa maelezo zaidi. Ada zetu zinaweza kubadilika na Paxful inahifadhi haki ya kurekebisha bei na ada zake wakati wowote.
  8. KUWASILISHA MIZOZO KUHUSU SHUGHULI ZA UNUNUZI NA UUZAJI KUPITIA MCHAKATO WA KUSULUHISHA MIZOZO WA PAXFUL

    1. Kuwasilisha Mizozo Kuhusu Shughuli za Ununuzi na Uuzaji. Mara nyingi, njia rahisi zaidi ya kusuluhisha mzozo ni kwa Wanunuzi na Wauzaji kuwasiliana, kushirikiana ili kubaini kilichotokea na kukubaliana kuhusu suluhisho. Mnunuzi na Muuzaji wasipokubaliana kuhusu suluhisho, timu ya usaidizi ya Paxful (“Huduma ya Usaidizi ya Paxful”) inaweza kusaidia. Mhusika yeyote anaweza kuanzisha mchakato wa kusuluhisha mzozo (“shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyo na mzozo” au “mzozo”) kulingana na shughuli husika ya ununuzi na uuzaji. Mizozo inaweza kuwasilishwa tu kwa shughuli za ununuzi na uuzaji ambazo hazijawekewa alama kuwa zimelipwa kikamilifu na Mnunuzi. Shughuli za ununuzi na uuzaji ambazo hazijawekewa alama kuwa zimelipwa kikamilifu na Mnunuzi, zilizoghairiwa na Mnunuzi, zilizoghairiwa kiotomatiki kwa sababu ya kukamilika kwa muda wake wa matumizi uliobainishwa kwenye ofa, ambazo tayari mizozo yake imewasilishwa na kusuluhishwa au ambapo Muuzaji ameachilia Mali Dijitali kwa Mnunuzi, kwa kawaida mizozo yake haiwezi kuwasilishwa, kurejeshwa au kubadilishwa.
    2. Mchakato wa Usuluhishaji wa Mzozo. Zifuatazo ni hatua ambazo Huduma ya Usaidizi ya Paxful huchukua ikiwa kuna mzozo wowote uliowasilishwa.

      1. Uanzishaji

        Unaweza kuanzisha mzozo kwa kuingia katika Akaunti yako ya Paxful, kufungua shughuli ya ununuzi na uuzaji ambayo ungependa kuwasilisha mzozo kuihusu kisha uchague kitufe “mzozo”. Kitufe cha “mzozo” kitaonekana tu kuwa kinatumika ikiwa shughuli ya ununuzi na uuzaji imewekewa alama kuwa imelipwa kikamilifu na Mnunuzi. Baada ya kuanzisha mzozo, utachagua aina ya mzozo kutoka kwa chaguo zilizotolewa na uelezee tatizo lililosababisha mzozo wako.

        Chaguo zilizotolewa za kubainisha mzozo wako ikiwa wewe ni Muuzaji ni zifuatazo:

        • Kifunga sarafu (yaani, Mnunuzi ambaye hajibu) – Mnunuzi ameweka alama kwenye shughuli ya ununuzi na uuzaji kama iliyolipwa kikamilifu, lakini hajibu na haitekelezi shughuli yoyote kwenye akaunti yake.
        • Tatizo la malipo – Mnunuzi anatekeleza shughuli kwenye akaunti yake na amejaribu kulipa, lakini kuna matatizo kwenye malipo yake.
        • Mengineyo – chaguo lililowazi ambapo unaweza kuelezea tatizo lililosababisha mzozo. Mnunuzi ataweza kuangalia maelezo yako.

        Chaguo zilizotolewa za kubainisha mzozo wako ikiwa wewe ni Mnunuzi ni zifuatazo:

        • Muuzaji ambaye hajibu – umelipa, lakini Muuzaji hajibu na hatekelezi shughuli yoyote kwenye akaunti yake.
        • Tatizo la malipo – umelipa, lakini Muuzaji adai kuwa kuna matatizo kwenye malipo na anakataa kuachilia Mali Dijitali.
        • Mengineyo – chaguo lililowazi ambapo unaweza kuelezea tatizo lililosababisha mzozo. Muuzaji ataweza kuangalia maelezo yako.
      2. Arifa

        Baada ya mzozo kuwasilishwa, Huduma ya Usaidizi ya Paxful itamtumia mhusika yule mwingine arifa kwa barua pepe na kwa kutuma ujumbe kupitia kipengele cha kupiga gumzo ya shughuli ya ununuzi na uuzaji kinachopatikana kwa Wanunuzi na Wauzaji kwenye Soko, ikimwarifu mhusika kama huyo kuwa mzozo umeanzishwa. Ikiwa mzozo umewasilishwa kwa mojawapo ya shughuli zako za ununuzi na uuzaji, Huduma ya Usaidizi ya Paxful itakueleza shughuli ya ununuzi na uuzaji ambayo mzozo umewasilishwa kuihusu.

      3. Jibu

        Kagua mzozo na utoe ufafanuzi kwa Paxful kuhusu kilichotokea. Jumuisha ushahidi wowote ulio nao wa kuunga mkono ufafanuzi wako, kama vile uthibitisho wa malipo, uthibitisho wa umiliki au uthibitisho kuwa umepokea au hujapokea malipo.

      4. Ukaguzi wa Paxful

        Shughuli za ununuzi na uuzaji ambazo mzozo umewasilishwa kuzihusu zitachunguzwa na Huduma ya Usaidizi ya Paxful na uamuzi utatolewa kulingana na ushahidi uliotolewa na wahusika wote wawili. Huduma ya Usaidizi ya Paxful husuluhisha mizozo kwa kutathmini vigezo mbalimbali jinsi ilivyobainishwa hapa chini katika Kifungu cha 8.

    3. Ukaguzi wa Mzozo. Wakati wa ukaguzi wa mzozo, Huduma ya Usaidizi ya Paxful inaweza kukupa maagizo ambayo unapaswa kuyafuata. Maagizo uliyopewa yanaweza kuhitaji utoe ushahidi wa ziada, kama vile uthibitishaji wa ziada wa kitambulisho, uthibitisho wa malipo, picha, rekodi ya sauti au ushahidi wowote wa video, au hati nyingine zozote ambazo Paxful itachukulia kuwa zinafaa na inaweza kukuhitaji utoe ushahidi kama huo katika kipindi fulani cha muda kilichobainishwa. Hatua ya kutofuata maagizo inaweza kusababisha uamuzi wa usuluhishaji wa mzozo uwe dhidi yako. Kwa kawaida, Huduma ya Usaidizi ya Paxful itatoa notisi kuhusu uamuzi iliyochukua kupitia kipengele cha kupiga gumzo ya shughuli ya ununuzi na uuzaji kwenye Soko katika kipindi cha siku 30 baada ya kupokea mzozo, lakini katika hali fulani, inaweza kuchukua muda mrefu.
    4. Hali ya kutojibu. Ukihusika katika shughuli ya ununuzi na uuzaji, ni muhimu uendelee kupatikana na kutekeleza shughuli kwenye akaunti yako kuanzia wakati ambapo shughuli ya ununuzi na uuzaji inaanzishwa hadi wakati ambapo itakamilishwa, kughairiwa au kusuluhishwa. Hii inamaanisha kuwa ni lazima uweze kujibu ombi la Huduma ya Usaidizi ya Paxful kuhusu shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyo na mzozo katika kipindi cha muda kilichobainishwa na Huduma ya Usaidizi ya Paxful au inaweza kuchukuliwa kuwa haupatikani na uamuzi wa mzozo unaweza kuchukuliwa dhidi yako.
    5. Malipo rejeshwa. Mhusika fulani anaweza kukumbana na hatari za ziada kulingana na njia ya kulipa iliyotumiwa kwa shughuli ya ununuzi na uuzaji, hata kama mchakato wa usuluhishaji wa mzozo wa Paxful utatoa uamuzi wa kumfaa mhusika kama huyo. Mchakato wa usuluhishaji wa mzozo uliobainishwa kwenye Makubaliano haya ni tofauti na suluhu zozote ambazo Mnunuzi au Muuzaji anaweza kupata kupitia njia ya kulipa iliyotumiwa kuhusiana na shughuli ya ununuzi na uuzaji. Paxful haiwajibiki katika kuanzisha na kushughulikia mizozo ya urejeshaji wa pesa na haiwajibiki ikiwa mhusika atafanya urejesho, kurejesha pesa au kuwasilisha mzozo dhidi ya shughuli ya ununuzi na uuzaji kupitia njia inayopatikana kwa mhusika huyo inayotolewa na njia ya kulipa iliyotumiwa katika shughuli hiyo ya ununuzi na uuzaji, ikiwa ni pamoja na baada ya mzozo kusuluhishwa.
    6. Usuluhishaji wa Mzozo. Shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyo na mzozo, mara nyingi husuluhishwa kwa Huduma ya Usaidizi ya Paxful kuhamishia Mali Dijitali inayohusika kwenye mzozo kwa Mnunuzi au Muuzaji wa shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyo na mzozo baada ya mchakato wa usuluhishaji wa mzozo kukamilika.

      Zifuatazo ni hali zilizochaguliwa ili kukupa maarifa kuhusu jinsi Paxful inaweza kusuluhisha shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyo na mzozo. Hii si orodha kamili. Usuluhishaji wa mzozo wowote utaathiriwa na maelezo ya kweli kuhusu mzozo na ushahidi uliotolewa na watumiaji.

      Huduma ya Usaidizi ya Paxful inaweza kusuluhisha mzozo kwa njia ya kumnufaisha Mnunuzi wakati ambapo angalau mojawapo ya vigezo vifuatavyo vimetimizwa:

      • Mnunuzi amelipa kulingana na maagizo ya awali yaliyotolewa na Muuzaji kwa mujibu wa ofa ya shughuli ya ununuzi na uuzaji na Mnunuzi ametoa uthibitisho wa kutosha kuwa malipo yalifanywa kulingana na maagizo hayo. Ni kitendo cha ukiukajii wa Makubaliano haya kwa Muuzaji kukataa kukamilisha shughuli ya ununuzi na uuzaji baada ya Mnunuzi kutimiza vigezo na masharti yote ya Muuzaji jinsi yalivyochapishwa wakati ambapo Mnunuzi alikubali na kulipia shughuli ya ununuzi na uuzaji.
      • Muuzaji hajibu na hajatoa jibu la kutosha katika kipindi cha muda kilichoombwa na Huduma ya Usaidizi ya Paxful.
      • Malipo yamelipwa kwa mtu mwingine anayehusika katika shughuli ya ununuzi na uuzaji au malipo yamelipwa kwa akaunti ya malipo ambayo haijasajiliwa kwa jina la Muuzaji.

      Huduma ya Usaidizi ya Paxful inaweza kusuluhisha mzozo kwa njia ya kumnufaisha Muuzaji wakati ambapo mojawapo ya vigezo vifuatavyo vimetimizwa:

      • Mnunuzi hajalipa, hajalipa malipo yote au hajalipa kulingana na maagizo ya awali yaliyotolewa na Muuzaji kwa mujibu wa ofa ya shughuli ya ununuzi na uuzaji.
      • Malipo yaliyolipwa na Mnunuzi yameshikiliwa, yamesimamishwa kwa muda, yamezuiliwa au yamesimamishwa na mtoa huduma au mchakataji. Hii ni pamoja na hali ambazo Mnunuzi amerejesha pesa za shughuli ya ununuzi na uuzaji au kuwasilisha mzozo kuhusu malipo kupitia benki au mtoaji wa kadi ya malipo.
      • Mnunuzi hajibu na hajatoa jibu la kutosha katika kipindi cha muda kilichoombwa na Huduma ya Usaidizi ya Paxful.
      • Malipo yamelipwa na mtu mwingine anayehusika katika shughuli ya ununuzi na uuzaji au malipo yamelipwa kutoka kwenye akaunti ya malipo ambayo haijasajiliwa kwa jina la Mnunuzi.

      Ikiwa Mnunuzi au Muuzaji wa shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyo na mzozo atatoa maelezo ya udanganyifu au hati za udanganyifu au kutoa madai ya uongo au kutumia mbinu za kilaghai, mzozo huo unaweza kusuluhishwa mara moja kinyume cha mtumiaji kama huyo na akaunti ya mtumiaji kama huyo inaweza kusimamishwa mara moja au kufungwa kwa hiari ya Huduma ya Usaidizi ya Paxful.

      Katika hali fulani ambapo hakuna mhusika yeyote aliyetimiza vigezo, au vinginevyo si dhahiri au si rahisi kubaini mhusika aliyetimiza vigezo vya usuluhishaji wa mzozo kwa hiari ya Paxful, Paxful inaweza kuamua kusuluhisha mzozo huo kwa kugawanya Mali Dijitali inayohusika katika mzozo baina ya Mnunuzi na Muuzaji kwa usawa au kwa njia isiyo sawa.

    7. Kukata rufaa. Ikiwa unaamini kuwa Paxful imesuluhisha mzozo kwa njia ambayo hailingani na Makubaliano haya, una haki ya kuomba kukata rufaa. Ili uombe kukata rufaa, unahitaji kutujulisha haraka iwezekanavyo kwa maandishi kwa kuwasiliana na huduma ya usaidizi kwa wateja ya Paxful kwa kipindi kisichozidi siku 10 baada ya kupokea notisi kuhusu uamuzi wa Huduma ya Usaidizi ya Paxful na utupatie maelezo na ushahidi wa kutosha unaounga mkono kesi yako ya kutuma ombi hilo. Rufaa yako inapaswa kubainisha kwa njia mahususi sababu inayofanya uamini kuwa Paxful ilisuluhisha mzozo huo visivyo kulingana na vigezo vya Makubaliano haya na utoe ushahidi wa uamuzi usio sahihi kama huo.

      Tafadhali kumbuka kuwa iwe ni wakati wa mchakato wa kushughulikia mzozo au wakati mwingine wowote unapotumia Huduma zetu, unapaswa kutumia lugha ya kawaida na uheshimu watumiaji wengine na Huduma ya Usaidizi ya Paxful. Angalia, “Kifungu cha 13 - Matumizi Yasiyoruhusiwa”.

    8. Hatima. Unakiri na kukubali kuwa uamuzi wa Paxful kuhusu mzozo wowote ni wenye kuondoa shaka, wa mwisho na usioweza kubatilishwa jinsi ilivyobainishwa kwenye Makubaliano haya. Paxful haitawajibika kwa Mnunuzi wala Muuzaji kuhusiana na maamuzi yake.
  9. ADA ZA KUTUMIA HUDUMA ZA PAXFUL

    1. Hulipishwi kutengeneza Pochi. Paxful hutoza ada za Huduma, ada zinazotumika zitaonyeshwa mapema kabla hujatumia Huduma yoyote ambayo inatozwa ada. Angalia “Ada za Paxful” kwa maelezo zaidi. Ada zetu zinaweza kubadilika na Paxful inahifadhi haki ya kurekebisha bei na ada zake wakati wowote.
  10. HAKUNA HAKI YA KUGHAIRI HUDUMA AU ADA YA WATENGENEZAJI WA SARAFU DIJITALI

    1. Ukitumia Huduma ambayo inatozwa ada, au uanzishe shughuli ya ununuzi na uuzaji iliyo na ada ya watengenezaji wa sarafu dijitali kupitia Huduma, hutakuwa na haki ya kurejeshewa au kufidiwa ada hiyo baada ya kuthibitisha kuwa ungependa kuendelea na shughuli ya ununuzi na uuzaji au kutumia Huduma.
  11. USIMAMISHAJI WA HUDUMA

    1. Tunaweza kwa hiari yetu sisi wenyewe na bila kukutoza gharama yoyote, kwa kutoa au bila kutoa notisi ya mapema na wakati wowote, kubadilisha au kusimamisha kwa muda au kusimamisha kabisa, sehemu yoyote ya Huduma yetu.
  12. KUSIMAMISHA AU KUFUNGWA KWA HUDUMA NA AKAUNTI; KUDHIBITI UFIKIAJI WA POCHI YAKO

    1. Tunaweza kwa hiari yetu sisi wenyewe, mara moja na bila kutoa notisi: (a) kusimamisha, kudhibiti au kukomesha ufikiaji wako wa Huduma yoyote au zote (ikiwa ni pamoja na kudhibiti ufikiaji wa Pochi yako), na/au (b) kuzima au kufuta akaunti yako ikiwa: (i) tunahitajika kufanya hivyo na sheria inayotumika, hati dhahiri ya kuitwa mahakamani inayotumika, agizo la mahakama au agizo lisiloweza kubatilishwa la mamlaka ya serikali; (ii) tunashuku kwa njia thabiti kuwa umekiuka au unaweza kukiuka Makubaliano haya; (iii) matumizi ya akaunti yako yanategemea usuluhishaji wa mzozo fulani mahakamani, uchunguzi au kesi inayosikilizwa na serikali na/au tunashuku kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutofuata sheria au kanuni inayohusishwa na shughuli za akaunti yako; (iv) washirika wetu wa huduma hawawezi kukuruhusu utumie huduma zao; (v) unachukua hatua yoyote ambayo tunachukulia kuwa inakwepa vidhibiti na utaratibu wetu au (vi) tunafikiria kuwa ni muhimu tufanye hivyo ili kujilinda, kuwalinda watumiaji wetu, ikiwa ni pamoja na wewe au wafanyakazi wetu dhidi ya hatari au hasara. Tukitekeleza haki zetu za kudhibiti au kuzuia ufikiaji wako wa Huduma, hatutawajibika kwa madhara yoyote ya kuzuia ufikiaji wako wa Huduma, ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji, uharibifu au usumbufu wowote unaoweza kupata kutokana na hatua hiyo.
    2. Tukisimamisha kwa muda au kufunga akaunti yako, kukomesha matumizi yako ya Huduma kwa sababu yoyote, au kudhibiti ufikiaji wa Pochi yako, tutajaribu kukutumia notisi kuhusu hatua tulizochukua isipokuwa agizo la mahakama au mchakato mwingine wa kisheria utuzuie kukutumia notisi kama hiyo. UNAKIRI KUWA UAMUZI WETU WA KUCHUKUA HATUA FULANI, IKIWA NI PAMOJA NA KUDHIBITI UFIKIAJI WA, KUSIMAMISHA KWA MUDA AU KUFUNGA AKAUNTI YAKO AU POCHI, UNAWEZA KULINGANA NA VIGEZO VYA SIRI AMBAVYO NI MUHIMU KATIKA UDHIBITI WETU WA HATARI NA TARATIBU ZA USALAMA. UNAKUBALI KUWA PAXFUL HAINA WAJIBU WOWOTE WA KUKUFICHULIA MAELEZO YA TARATIBU ZAKE ZA UDHIBITI WA HATARI NA USALAMA. Ikiwa tutasimamisha kwa muda akaunti yako au ufikiaji wa Pochi yako, tutaondoa hali ya kusimamishwa kwa muda haraka iwezekanavyo baada ya sababu ya kusimamishwa kwa muda kusuluhishwa, hata hivyo hatuna wajibu wowote wa kukuarifu kuhusu wakati ambapo (ikiwa upo) hali hiyo ya kusimamishwa kwa muda itaondolewa.
    3. Ikiwa unashikilia Mali Dijitali kwenye Pochi yako ya Paxful na hujakuwa ukitekeleza shughuli zozote kwenye akaunti yako kwa kipindi cha muda kinachoagizwa na sheria inayotumika, tunaweza kuhitajika kuripoti Mali Dijitali kama hiyo iliyosalia kwenye akaunti yako kama mali isiyo na mwenyewe kwa mujibu wa sheria za uerejeshaji wa mali kwa serikali na mali isiyo na mwenyewe. Hali hii ikitokea, tutatumia juhudi zinazofaa ili kukutumia notisi iliyoandikwa. Usipojibu notisi kama hiyo katika kipindi cha siku saba (7) za kazi baada ya kuipokea, au jinsi inavyohitajika na sheria, tutahitajika kupeana Mali yoyote Dijitali kama hiyo kwa mamlaka inayotumika kama mali isiyo na mwenyewe. Tunahifadhi haki ya kutoza ada ya akaunti isiyotumika au ada nyingine za usimamizi kutoka kwa Mali Dijitali kama hiyo isiyo na mwenyewe jinsi inavyoruhusiwa na sheria inayotumika.
    4. We reserve the right to reverse internally received Digital Assets to your Paxful Wallet back to the originating account if the owner of the originating account successfully demonstrates that the Digital Assets were transferred to your Paxful Wallet in error, and if there has been no activity in your account for a period of 24 months. If this occurs, we will use reasonable efforts to provide written notice to you. If you fail to respond to any such notice within 14 days, we may be required to reverse Digital Assets to the owner of the originating account.
  13. MATUMIZI YASIYORUHUSIWA

    1. Unapofikia au kutumia Huduma, unakubali kuwa utatumia Huduma kwa mujibu wa vigezo na masharti yaliyo kwenye Makubaliano haya (ikiwa ni pamoja na Sera ya Faragha) na kutotekeleza kitendo chochote cha kinyume cha sheria, na kuwa unawajibika kikamilifu kwa matendo yako unapotumia Huduma zetu. Kando na yaliyotajwa, unakubali kuwa:
      1. hutatumia Huduma zetu kwa namna yoyote ambayo inaweza kuingilia, kukatiza, kuathiri vibaya au kuzuia watumiaji wengine kutofurahia Huduma zetu kikamilifu, au ambayo inaweza kuharibu, kuzima, kulemeza au kudhoofisha utendakazi wa Huduma zetu kwa namna yoyote;
      2. hutajihusisha kwenye shughuli yoyote ambayo inaweza kukiuka, au kusaidia katika ukiukaji wa, sheria, kanuni au agizo lolote, mipango ya vikwazo inayotumika kwenye nchi ambako tunafanya biashara au shughuli zetu, au ambayo itahusisha mapato ya shughuli yoyote isiyo halali; kuchapisha, kusambaza au kueneza maelezo au nyenzo yoyote isiyo halali;
      3. hutaathiri uwezo wa mtumiaji mwingine kufikia au kutumia Huduma yetu yoyote; hutaharibu jina, kutumia vibaya, kupokonya, kusumbua, kunyemelea, kutishia au kukiuka au kuingilia haki halali (kama vile, wala si tu, haki za faragha, kujulikana na uvumbuzi) za watu wengine; hutachochea, kutishia, kuwezesha, kuendeleza au kuhimiza chuki, ubaguzi wa kimbari au vitendo vya kuzua vurugu dhidi watu wengine; hutapata au kukusanya maelezo kutoka kwa Tovuti yetu kuhusu watumiaji wengine;
      4. hutajihusisha kwenye shughuli yoyote ambayo matokeo yake ni kulaghai, kuharibu jina au kusababisha uharibifu wowote kwa Paxful au kwa watumiaji wetu; au kutoa maelezo yoyote ya uongo, yasiyo sahihi, ya udanganyifu au yanayopotosha kwa Paxful au kwa mtumiaji mwingine kuhusiana na Huduma zetu au jinsi inavyobainishwa au kuombwa kwa mujibu wa Makubaliano haya;
      5. hutaweka virusi vyovyote kwenye Huduma, Trojan, worms, logic bombs au nyenzo nyingine hatari; hutatumia roboti, buibui, kitaambaji, kidukuzi au mbinu nyingine za kiotomatiki au kiolesura kisichotolewa nasi ili kufikia Huduma zetu au kuchopoa data; hutajaribu kukwepa mbinu zozote za kuchuja maudhui tunazotumia, au kujaribu kufikia huduma yoyote au sehemu ya Huduma zetu ambayo hurusiwi kufikia; au kuweka ofa au matangazo yoyote mahali popote kwenye Soko la Paxful ambayo yatawezesha ununuzi na uuzaji wa Mali Dijitali nje ya Huduma za Paxful;
      6. hutajihusisha kwenye shughuli za ununuzi na uuzaji zinazohusisha bidhaa ambazo zinaingilia au kukiuka haki yoyote ya hakimiliki, alama ya biashara, haki ya kujulikana au faragha au haki nyingine yoyote ya umiliki inayopatikana kwenye sheria, au nyenzo nyingine zilizo na leseni bila idhini inayofaa kutoka kwa wamiliki wa haki; kutumia mali ya uvumbuzi ya Paxful, jina au nembo, ikiwa ni pamoja na kutumia alama za biashara au za huduma za Paxful, bila ruhusa ya mapema iliyoandikwa nasi au kwa namna ambayo inasababisha madhara kwa Paxful au kwa chapa ya Paxful; kitendo chochote ambacho kinaashiria uidhinishaji usio wa kweli na au ushirikiano na Paxful; au kutengeneza programu zozote za watu wengine ambazo zinatumia Huduma zetu bila ruhusa ya mapema iliyoandikkwa nasi; au
      7. hutahimiza au kushawishi mtu mwingine yeyote kushiriki kwenye shughuli zozote ambazo haziruhusiwi chini ya Kifungu hiki cha 13.
  14. HAKI ZA UVUMBUZI

    1. Tunakupa leseni inayodhibitiwa, isiyo ya kipekee na isiyoweza kuhamishiwa kwa mtu mwingine, kulingana na vigezo na masharti yaliyo kwenye Makubaliano haya, ya kufikia na kutumia mara kwa mara Huduma, Tovuti na maudhui yanayohusiana, nyenzo, maelezo (kwa ujumla, “Maudhui”) kwa madhumuni yaliyoidhinishwa na Paxful pekee. Matumizi mengine ya Tovuti au Maudhui hayaruhusiwi kabisa na haki, jina na nia nyingine zote kwenye Huduma, Tovuti au Maudhui ni mali ya Paxful pekee. Unakubali kuwa hutanakili, kutuma, kusambaza, kuuza, kutoa leseni, kufanya utafiti wa kihandisi, kurekebisha, kuchapisha au kushiriki katika utumaji au uuzaji wa, kuunda miigo ya kazi kutoka kwa, au kutumia Maudhui yoyote kwa ukamilifu au kwa sehemu yake, kwa namna nyingine yoyote isiyo ya haki, bila ruhusa ya mapema iliyoandikwa na Paxful. Hupaswi kunakili, kuiga au kutumia alama zozote za biashara, alama zilizosajiliwa, nembo au mali yoyote ya uvumbuzi ya Paxful bila ruhusa ya mapema iliyoandikwa na Paxful.
    2. Ingawa tunakusudia kutoa maelezo sahihi na kwa wakati kwenye Tovuti ya Paxful, Tovuti yetu (ikiwa ni pamoja, wala si tu, Maudhui) huenda isiwe na maelezo yasiyo sahihi, kamilifu au yaliyosasishwa na yanaweza pia kujumuisha hitilafu za kuchapishwa au za kiufundi. Katika juhudi za kuendelea kukupa maelezo yaliyo sahihi na kamilifu zaidi kadri iwezekanavyo, maelezo yanaweza kubadilishwa au kusasishwa mara kwa mara bila kutoa notisi, ikiwa ni pamoja na, wala si tu, maelezo yanayohusiana na sera, bidhaa na Huduma zetu. Pia, unapaswa kuthibitisha maelezo yote kabla ya kuyategemea, na maamuzi yote unayofanya kulingana na maelezo yaliyo kwenye Tovuti ya Paxful ni wajibu wako mwenyewe na hatutawajibika kwa maamuzi kama hayo. Maelezo yanayotolewa na watu wengine ni ya madhumuni ya kutoa maelezo pekee na Paxful haitoi uwakilishaji au dhamana zozote kwa usahihi wa maelezo kama hayo. Viungo vya kuelekeza kwa nyenzo za watu wengine (ikiwa ni pamoja na, wala si tu, tovuti) vinaweza kutolewa kama huduma ya ziada lakini hatuvidhibiti. Unakiri na kukubali kuwa hatuwajibiki kwa kipengele chochote cha maelezo, maudhui au Huduma zinazopatikana kwenye nyenzo yoyote ya watu wengine au tovuti zozote za watu wengine zinazowezza kufikiwa au zilizounganishwa kwenye Tovuti ya Paxful.
  15. MAONI NA MAWASILISHO YA MTUMIAJI

    1. Paxful inajitahidi kila wakati kuboresha Huduma zake na Tovuti. Ikiwa una mawazo au mapendekezo kuhusiana na maboresho au vipengee vya kuongezwa kwenye Huduma za Paxful au Tovuti, Paxful ingependa kupata maoni yako; hata hivyo, mawasilisho yoyote yatategemea vigezo na masharti yaliyo kwenye Makubaliano haya.
    2. Ufichuaji wowote wa mawazo au maoni, au nyenzo yoyote inayohusiana kwa Paxful au kwa kampuni zake tanzu, kampuni kuu au kampuni zake washirika zozote, au kwa maofisa, wakurugenzi, wasimamizi, wanachama, wadau, wafanyakazi na maajenti wake wowote, au kwa warithi, wawakilishi na wakabidhiwa wake wowote (kila mmoja anarejelewa kama “Mshirika wa Paxful” na kwa ujumla Washirika wa Paxful”) hautategemea wajibu wowote wa kudumisha usiri au matarajio ya kufidiwa, kwa vyovyote vile.
    3. Kwa kuwasilisha wazo au maoni au nyenzo yoyote inayohusiana ambayo itategemea haki za mali ya uvumbuzi (“Kazi”) kwa Paxful au kwa Mshirika yeyote wa Paxful, unaipa Paxful, kulingana na Kazi iliyowasilishwa, leseni isiyo ya kipekee, ya kudumu ya kimataifa isiyolipishwa ya kutumia maudhui yote ya mawazo na maoni kama hayo, kwa madhumuni yoyote. Pia, unasalimisha haki zozote za umiliki wa Kazi hiyo ulizo nazo kwa kiwango cha juu zaidi kinachoruhusiwa chini ya sheria ya Marekani na uwakilisha na kutoa dhamana kwa Mshirika wa Paxful kama huyo kuwa Kazi hiyo ni kazi yako halisi, kuwa hakuna mtu mwingine aliye na haki ya umiliki kwenye Kazi hiyo na kuwa Washirika wote wa Paxful hawalipishwi ili kutumia Kazi hiyo na kutumia nyenzo zinazohusiana wakipenda, jinsi ilivyotolewa au jinsi ilivyorekebishwa na Mshirika yeyote wa Paxful, bila kuomba ruhusa au leseni kutoka kwa mtu mwingine yeyote.
    4. Unakubali zaidi kuwa Paxful inaweza kutoa leseni ndogo kwa Washirika wake wowote ya kutumia Kazi na nyenzo yoyote uliyowasilisha kwa njia yoyote.
    5. Tuna haki ya kuondoa chapisho lolote unaloweza kuchapisha kwenye Tovuti, kwa hiari yetu sisi wenyewe, bila kutoa onyo wala sababu.
  16. JINSI YA KUWASILIANA NASI

    Tunapendekeza kuwa utembelee ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kabla ya kuwasiliana nasi. Ikiwa ukurasa wa Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara hauna maelezo unayotafuta, Paxful inatoa huduma ya usaidizi wakati wowote. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia wijeti yetu ya usaidizi inayopatikana kwenye ukurasa wa Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.

  17. HALI ISIYOEPUKIKA

    1. Hatutawajibika kwa ucheleweshaji, hali ya Huduma kuacha kufanya kazi au kukatizwa ambayo inatokana moja kwa moja na chanzo au hali yoyote tusiyoweza kuidhibiti, ikiwa ni pamoja na, wala si tu, mabadiliko makubwa ya soko, ucheleweshaji au hali yoyote ya huduma kuacha kufanya kazi inayotokana na kitendo chochote cha Mungu, kitendo cha mamlaka za raia au jeshi, kitendo cha magaidi, usumbufu wa raia, vita, mgomo au mzozo mwingine wa kikazi, moto, kukatizwa kwa huduma za mawasiliano ya simu au huduma za mtandao au huduma za mtoa huduma, hali ya kifaa na/au programu kuacha kufanya kazi, balaa nyingine au tukio jingine lolote ambalo hatuwezi kulidhibiti na ambalo halitaathiri matumizi au uwezo wa kutekelezwa kwa vifungu vyovyote vilivyosalia.
  18. HALI YA MAKUBALIANO

    1. Makubaliano haya yanajumuisha makubaliano yote baina yako na Paxful kulingana na suala husika la vigezo na masharti yaliyo kwenye Makubaliano haya na Makubaliano haya yanaghairi na yanachukua nafasi ya maelewano na makubaliano yoyote ya awali baina yako na Paxful kulingana na suala hilo husika. Hupaswi kumkabidhi mtu yeyote haki au majukumu yako yoyote yaliyo kwenye Makubaliano haya bila ruhusa ya mapema iliyoandikwa nasi.