Notisi ya Faragha ya Paxful, Inc.

Paxful, Inc. (inayorejelewa pia kama “Paxful,” “sisi,” “nasi,” au “yetu”) huchukua hatua za kulinda faragha yako. Kwenye Notisi hii ya Faragha (“Notisi”), tunaelezea aina za maelezo ya kibinafsi tunayoweza kukusanya kutoka kwako kuhusiana na utumiaji wako wa tovuti zetu ikiwa ni pamoja na, wala si tu, https://paxful.com/, Pochi ya Paxful, mfumo wetu wa mtandaoni wa biashara ya bitcoin, programu ya kifaa cha mkononi, kurasa za mitandao ya kijamii au mali nyingine za mtandaoni (kwa ujumla, “Tovuti”), au unapotumia bidhaa, huduma, maudhui, mali, teknolojia au vipengele vyovyote tunavyotoa (kwa ujumla, “Huduma”).

Notisi hii imetungwa ili kukusaidia upate maelezo kuhusu desturi zetu za faragha na kukusaidia uelewe chaguo zako za faragha unapotumia Tovuti na Huduma zetu. Tafadhali kumbuka kuwa Huduma tunazotoa zinaweza kutofautiana kulingana na eneo.

Kwa madhumuni yote, toleo la lugha ya Kiingereza la notisi hii ya faragha litakuwa zana halisi ya usimamizi. Ikiwa ukinzani wowote utatokea kati ya toleo la lugha ya Kiingereza la notisi hii ya faragha na tafsiri yoyote itakayofuata kwa lugha nyingine yoyote, toleo la lugha ya Kiingereza litatumika.

Maelezo ya kibinafsi tunayokusanya

Tunakusanya maelezo yanayokuhusu (“Data ya Kibinafsi”) kuhusiana na utumiaji wako wa Tovuti, Huduma zetu au vinginevyo kwa muktadha wa uhusiano wetu nawe. Aina za Data za Kibinafsi tunazoweza kukusanya kutoka kwako zinaweza kuwa ni pamoja na:

Data Kuhusu Wasifu, ikiwa ni pamoja na:

  • Jina
  • Anwani ya Barua Pepe
  • Namba ya simu
  • Nchi
  • Anwani Kamili
  • Tarehe ya Kuzaliwa

Maelezo ya Akaunti ya Paxful, ikiwa ni pamoja na:

  • Jina la mtumiaji
  • Maelezo ya Wasifu wa Mtumiaji kwenye sehemu ya “Bio”
  • Picha ya Wasifu
  • Tarehe ya Kujisajili
  • Sarafu Chaguo-msingi
  • Saa za Eneo
  • Lugha Chaguo-msingi

Shughuli za Akaunti ya Paxful, ikiwa ni pamoja na:

  • Ujumbe wa Gumzo la Uchuuzi (ambao unaweza kuwa na maelezo kifedha ikiwa utazituma kwa wauzaji)
  • Viambatisho vya Gumzo la Uchuuzi
  • Shughuli za Biashara
  • Historia ya Miamala
  • Jina la Mshirika
  • Kitambulisho cha Mshirika
  • Kiungo cha Mshirika
  • Shughuli za Ununuzi na Uuzaji za Mshirika
  • Ofa Zilizotengenezwa
  • Vigezo vya Ofa
  • Maelekezo ya Uuzaji
  • Arifa za Akaunti
  • Hali ya Akaunti

Data inayohusiana na pochi yako ya mali Dijitali, ikiwa ni pamoja na:

  • Funguo za Faragha
  • Funguo Zisizo za Faragha
  • Salio la Pochi
  • Miamala iliyopokewa
  • Miamala iliyotumwa

Data Iliyokusanywa kuhusiana na Utiifu wa masharti ya “Know Your Customer” (KYC), ikiwa ni pamoja na:

  • Kitambulisho kinachotolewa na serikali
  • Uthibitisho wa Anwani
  • Picha, ikiwa utaamua kutupatia
  • Video, ikiwa utaamua kutupatia

Data ya Matumizi ya Kifaa na Tovuti, ikiwa ni pamoja na:

  • Anwani ya IP
  • Kitambulisho cha Vidakuzi na/au vitambulishi vingine vya kifaa
  • Maelezo yanayohusiana na ufikiaji wako kwenye Tovuti, kama vile maelezo ya kifaa, tarehe na wakati
  • Lugha unazopendelea
  • Maelezo kuhusu vitendo ulivyotekeleza wakati wa kutumia Tovuti

Data ya matumizi ya programu ya rununu, ikijumuisha:

  • Data ya kipindi: Anwani ya IP, toleo la mfumo wa uendeshaji, chapa na muundo wa kifaa, vitambulishi vya kipekee vya kifaa, kivinjari kilichotumiwa, maelezo kuhusu wakati Programu ilifikiwa, jina na vigezo vya muunganisho wa mtandao.
  • Taarifa kuhusu programu zilizosakinishwa kwenye kifaa cha Mtumiaji (metadata kutoka kwa programu): jina la programu, kitambulisho cha programu na toleo, kitambulisho cha kifaa na jumla ya idadi sahihi. Kugundua programu hasidi na kulinda watumiaji dhidi ya ulaghai ndizo sababu kuu za kukusanya taarifa kuhusu programu zilizosakinishwa.
  • Maelezo kuhusu hatua zilizotekelezwa wakati wa kutumia programu ya simu
  • Data ya uchunguzi wa hitilafu za kuharibika na za programu

Jinsi tunavyotumia data yako

Madhumuni ya kibiashara yanayofanya tukusanye, tutumie, tuhifadhi na tushiriki Data yako ya Kibinafsi yanaweza kuwa ni pamoja na:

  • Kutoa Huduma kupitia kuendesha Tovuti, ikiwa ni pamoja na:
    • Kusajili, kutengeneza na kudumisha akaunti yako;
    • Kuthibitisha utambulisho wako na/au kufikia akaunti yako au kusaidia wauzaji kuthibitisha utambulisho wako;
    • Kuanzisha, kuwezesha, kushughulikia na/au kutekeleza shughuli za miamala;
    • Kuwasiliana nawe kuhusiana na akaunti yako au Huduma yoyote unayotumia;
    • Kutekeleza ukaguzi wa kustahiki kupokea mikopo, KYC au ukaguzi mwingine kama huo;
    • Kutathmini maomi; au
    • Kulinganisha maelezo kwa madhumuni ya kuhakikisha usahihi na uthibitishaji.
  • Kudhibiti hatari na kukulinda wewe, watu wengine na Tovuti na Huduma zetu.
  • Ili kukupa hali ya utumiaji inayokufaa zaidi na kutekeleza mapendeleo yako.
  • Ili kuelewa vizuri wateja na jinsi wanavyotumia Tovuti na Huduma zetu.
  • Ili kukupa matangazo.
  • Ili kukupa Huduma, ofa na matangazo yanayokufaa zaidi kwenye Tovuti yetu na kwenye tovuti za watu wengine.
  • Ili kukupa chaguo, vipengele na ofa zinazolingana na eneo.
  • Ili kutii sera na majukumu yetu, ikiwa ni pamoja na, wala si tu, ufichuaji na majibu kulingana na maombi yoyote kutoka kwa mamlaka za utekelezaji wa sheria na/au wasimamizi kwa mujibu wa sheria yoyote inayotumika, kanuni, agizo la serikali au la kisheria, mamlaka ya usimamizi yenye uwezo thabiti wa kutekeleza sheria, ombi la kupata ushahidi au michakato yoyote ya kisheria kama hiyo.
  • Ili kusuluhisha mizozo, kukusanya ada au kutatua matatizo.
  • Ili kukupa huduma kwa wateja au kuwasiliana nawe.
  • Ili kudhibiti biashara yetu.

Tunaweza pia kuchakata Data ya Kibinafsi kwa kazi zingine kulingana na idhini yako panapohitajika na sheria inayotumika.

Vyanzo tunazotumia kukusanya data ya kibinafsi

Tunakusanya Data ya kibinafsi kutoka kwa vyanzo kadhaa, ikiwa ni pamoja na

  • Moja kwa moja kutoka kwako: Tunakusanya Data ya kibinafsi moja kwa moja kutoka kwako unapotumia Tovuti au Huduma zetu, unapowasiliana nasi au unaposhirikiana nasi moja kwa moja.
  • Kutoka kwa watoa huduma na/au wachakataji wa data wanaotusaidia kuendesha Tovuti au Huduma zetu: Tunaweza kuwasiliana na watoa huduma ili watusaidie kuwezesha huduma za Tovuti au kutoa Huduma zetu kwako, kwa maelekezo yetu au kwa niaba yetu. Watoa huduma hawa wanaweza kukusanya maelezo kukuhusu na kutupatia maelezo hayo.
  • Kutoka kwa watumiaji wengine kwenye Tovuti ya Paxful au kutoka kwa washirika waliojumuishwa kwenye Huduma au Tovuti ya Paxful: Watumiaji wengine wanaweza kutupatia maelezo kukuhusu yanayohusiana na gumzo au shughuli za ununuzi na uuzaji. Washirika pia wanaweza kutupatia maelezo kukuhusu yanayohusiana na mawasiliano au miamala unayofanya na washirika kama hao.
  • Kutoka kwa watu wengine ambao wanaweza kutusaidia kuthibitisha utambulisho, kuzuia utapeli na kulinda usalama wa shughuli za miamala.
  • Kutoka kwa watu wengine ambao wanaweza kutusaidia kutathmini ustahiki wako wa kupata mikopo au rekodi yako ya kifedha.
  • Kutoka kwa watu wengine ambao wanaweza kutusaidia kuchanganua Data ya Kibinafsi, kuboresha Tovuti au Huduma au hali yako ya utumiaji, kutangaza bidhaa au huduma au kukupa matangazo na ofa.
  • Kutoka kwa mifumo ya mitandao ya kijamii, ikiwa unawasiliana nasi kupitia mitandao ya kijamii.

Jinsi tunavyoshiriki data

Katika hali fulani, tunaweza kufichua Data ya Kibinafsi fulani kwa watu wengine. Aina za watu ambao tunashiriki nao Data ya kibinafsi ni pamoja na:

  • Watoa huduma na/au wachakataji wa data: Tunaweza kushiriki Data ya Kibinafsi na watoa huduma wengine ambao hutekeleza huduma na shughuli kulingana na maelekezo yetu na kwa niaba yetu. Watoa huduma hawa wengine wanaweza, kwa mfano, kukupa Huduma, kuthibitisha utambulisho wako, kusaidia katika kuchakata miamala, kukutumia matangazo ya bidhaa na Huduma zetu au kukupa huduma ya usaidizi kwa wateja.
  • Wahusika wengine wa shughuli za ununuzi na uuzaji, kama vile wauzaji: Tunaweza kushiriki maelezo na washiriki wengine wa miamala yako, ikiwa ni pamoja na watumiaji wengine ambao unanunua mali dijitali kutoka kwao.
  • Taasisi za fedha na kampuni nyingine zinazohusika katika kukusaidia kufanya malipo yanayohusiana na shughuli zako za miamala
  • Washirika ambao wanaelekezwa kutoka kwenye Tovuti yetu
  • Kutoka kwa watu wengine kwa madhumuni yetu ya kibiashara au jinsi inavyoruhusiwa au inavyohitajika na sheria, ikiwa ni pamoja na:
    • Ili kutii majukumu yoyote ya kisheria, usimamizi au ya kimkataba au kutii mchakato wowote wa kisheria au usimamizi (kama vile agizo la mahakama linalotumika au hati ya kuitwa mahakamani);
    • Ili kuanzisha, kutekeleza au kulinda madai ya kisheria;
    • Kulingana na ombi la shirika la serikali, kama vile mamlaka ya kutekeleza sheria au agizo la kisheria;
    • Ili kutekeleza Vigezo vya Huduma vya Tovuti yetu au sera zetu za ndani;
    • Ili kuzuia madhara halisi au hasara ya kifedha, inayohusiana na uchunguzi wa shughuli haramu halisi au inayodhaniwa au vinginevyo, kulinda haki, mali au usalama wetu au watu wengine;
    • Ili kuwezesha ununuzi au uuzaji wa sehemu au biashara yote ya Paxful. Kwa mfano, kwa kushiriki data na kampuni tunayopanga kuungana nayo au kununuliwa nayo; au
    • Ili kusaidia katika mchakato wetu wa ukaguzi wa mahesabu, kutii masharti na shughuli za usimamizi za shirika.

Utumaji wa data nje ya nchi

Tafadhali kumbuka kuwa tunaweza kutuma Data ya kibinafsi tunayokusanya kukuhusu kwa nchi zingine kando na nchi ambako tulikusanya maelezo hayo. Huenda nchi hizo hazina sheria za ulinzi wa data zinazofanana na za nchi ambako tulikusanya maelezo yako. Tunapotuma Data yako ya kibinafsi kwa nchi zingine, tunachukua hatua zilizobuniwa ili kuhakikisha kuwa utumaji huo unalingana na sheria inayotumika.

Vidakuzi na matangazo ya mtandaoni

  • Kidakuzi ni faili ndogo ya maandishi ambayo tovuti huhifadhi kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi unapotembelea tovuti.
  • Tovuti yetu hutumia vidakuzi na teknolojia za ufuatiliaji ili kufanya kazi na kuonyesha matangazo ambayo yanaweza kukuvutia. Kwa maelezo zaidi, tafadhali rejelea Sera yetu ya Vidakuzi.
  • Paxful inaweza kushirikiana na mitandao ya matangazo ya watu wengine ili kuonyesha matangazo kwenye Tovuti ya Paxful au kwenye tovuti za watu wengine. Tovuti hizi na mitandao ya matangazo ya watu wengine haidhibitiwi na Paxful. Washirika wa mitandao ya matangazo hutumia teknolojia za data kukusanya maelezo kuhusu shughuli zako za mtandaoni ili kukuonyesha matangazo yanayokufaa kulingana na mambo yanayokuvutia. Ikiwa hungependa maelezo haya yatumiwe kwa madhumuni ya kukuonyesha matangazo yanayokufaa, unaweza kujiondoa kwa kutembelea:

Tafadhali kumbuka kuwa hatua hii haikuzuii kuonyeshwa matangazo; utaendelea kupokea matangazo ya kawaida ambayo hayalingani na mambo mahususi yanayokuvutia. Unaweza kudhibiti matumizi ya vidakuzi katika kiwango cha kivinjari chako mwenyewe. Usipokubali vidakuzi, bado unaweza kutumia Tovuti yetu, lakini huenda hutaweza kutumia baadhi ya vipengele au maeneo ya Tovuti yetu.

Uhifadhi wa data

Tunahifadhi Data ya Kibinafsi kwa kipindi kinachohitajika kwa madhumuni ya ukusanyaji wa data hiyo au kwa vipindi vinavyohitajika na sheria inayotumika. Hii inaweza kujumuisha kuhifadhi Data ya Kibinafsi kwa vipindi vinavyofuata miamala. Sisi hujitahidi kufuta Data yako ya Kibinafsi ikiwa haihitajiki tena kwa madhumuni yoyote ya kibiashara yaliyoelezewa hapo juu.

Usalama wa data

Paxful imeweka mbinu za ulinzi zilizobuniwa ili kulinda Data yako ya Kibinafsi, ikiwa ni pamoja na mbinu zilizobuniwa ili kuzuia kupotea, kutumiwa vibaya na ufikiaji au ufichuaji wa Data ya Kibinafsi bila idhini. Hata hivyo, Paxful haiwezi kuhakikisha au kutoa hakikisho la usalama au usiri wa maelezo unayotutumia kupitia Intaneti au muunganisho wa mtandao pasiwaya. Kila wakati, hatua ya kutuma data kupitia Intaneti ina hatari fulani, hata kama Paxful hujitahidi kulinda data pindi inapoipokea.

Watoto walio na umri wa chini ya miaka 18

Tovuti ya Paxful haikusudiwi kutumiwa na watoto walio na umri wa chini ya miaka 18. Hatukusanyi kimakusudi data kutoka kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 18 bila idhini iliyothibitishwa ya mzazi. Tukifahamu kuwa tumekusanya maelezo, ikiwa ni pamoja na Data ya Kibinafsi, kutoka kwa mtu aliye na umri wa chini ya miaka 18 bila idhini ya mzazi, tutafuta maelezo hayo mara moja.

Marekebisho ya notisi ya faragha

Paxful inahifadhi haki za kubadilisha Notisi hii mara kwa mara. Tutakuarifu kuhusu marekebisho ya Notisi hii kwa kuchapisha toleo lililorekebishwa la Notisi hii hapa, kupitia barua pepe au kupitia kwa notisi kuu kwenye ukurasa wa mwanzo wa Tovuti ya Paxful. Tunakuhimiza uangalie Tovuti mara kwa mara ili uone ikiwa kuna mabadiliko yoyote.

Wasiliana nasi

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Notisi hii au ungependa kutuuliza kuhusu Data ya Kibinafsi au faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia: [email protected]

Nyongeza ya EEA

Ufumbuzi ufuatao unatumika kwa, na umekusudiwa hasa kwa, watu wanaoishi katika nchi washirika wa Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA).

Mdhibiti Data

Mdhibiti wa Data yako ya kibinafsi ni Paxful, Inc.

Misingi ya Kisheria ya Kuchakata Data ya Kibinafsi

  • Kiwango ambacho tunatumia Data ya Kibinafsi ili kutekeleza majukumu ya kimkataba au kushughulikia maombi unayotuma kuhusiana na mkataba, Kifungu cha 6(1)(b) cha Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (“GDPR”) ndicho msingi wa kisheria wa uchakataji wetu wa data.
  • Kwa kiwango ambacho tunatumia Data ya Kibinafsi ili kufuata masharti ya kisheria chini ya sheria ya EU au Nchi Mwanachama, Kifungu cha 6(1)(c) cha GDPR ndicho msingi wa kisheria wa uchakataji wetu wa data.
  • Kwa kiwango ambacho tunatumia Data ya Kibinafsi ili kulinda maslahi muhimu ya watu binafsi, Kifungu cha 6(1)(d) cha GDPR ndicho msingi wa kisheria wa uchakataji wetu wa data.
  • Kwa kiwango ambacho tunatumia Data ya Kibinafsi ili kutimiza maslahi yetu halali ya kibiashara, Kifungu cha 6(1)(f) cha GDPR ndicho msingi wa kisheria wa uchakataji wetu wa data. Orodha ya maslahi yetu halali ya kibiashara inapatikana katika sehemu iliyo hapo juu inayoitwa “Jinsi Tunavyotumia Data Yako”.

Haki za Ulinzi wa Data za Ulaya

Sheria ya ulaya inakupatia haki fulani kuhusiana na Data yako ya Kibinafsi, ikiwa ni pamoja na:

  • Haki ya kuomba kufikia na kurekebisha Data yako ya Kibinafsi.
  • Haki ya kuomba Paxful ifute Data mahususi ya Kibinafsi inayokuhusu.
  • Haki ya kuhamisha data, ambayo ni pamoja na haki ya kuomba kuwa Data mahususi ya Kibinafsi uliyotoa ihamishwe kutoka kwetu hadi kwa mdhibiti mwingine wa data.
  • Haki ya kuondoa idhini yoyote uliyoipa Paxful ya kukusanya, kutumia au kushiriki data yako wakati wowote. Tafadhali kumbuka kuwa hatua ya kuondoa idhini yako haiathiri uhalali wa Paxful wa kuchakata Data yako ya Kibinafsi kabla ya kuondoa idhini yako.
  • Haki ya kukataa Paxful ichakate Data yako ya Kibinafsi, kulingana na misingi mahususi ya hali yako.
  • Haki ya kuomba kuwa Paxful izuie uchakataji wa Data yako ya Kibinafsi, ikiwa umetimiza hali fulani za kisheria za uzuiaji.
  • Haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka ya usimamizi ya Ulaya.

Tafadhali kumbuka kuwa sheria inayotumika inaweza kutoa hali za kipekee za kutotumiwa kwa haki hizi, kuruhusu Paxful kukataa ombi lako au kuruhusu Paxful kuongeza kipindi chake cha kushughulikia ombi lako. Paxful inaweza pia kuwasiliana nawe ili kuthibitisha utambulisho wako, jinsi inavyoruhusiwa na sheria, kabla ya kushughulikia ombi lako. Ili utumie mojawapo ya haki hizi, tafadhali wasiliana nasi jinsi ilivyobainishwa katika sehemu iliyo hapo inayoitwa “Wasiliana Nasi”.

Utumaji wa Nje ya Nchi

Tunaweza kutuma Data ya Kibinafsi inayohusiana na wakazi wa EEA kwa nchi ambazo si wanachama wa Tume ya Ulaya ili kutoa ulinzi wa kutosha, ikiwa ni pamoja na Marekani. Kwa utumaji kama huo, Paxful imeweka mbinu za ulinzi zilizobuniwa ili kuhakikisha kuwa Data yako ya Kibinafsi inalindwa kwa kiwango cha kutosha. Ikiwa wewe ni mkazi wa EEA, Paxful itatuma tu Data yako ya Kibinafsi ikiwa: nchi ambako Data ya Kibinafsi itatumwa imepewa uamuzi wa utoshelevu kutoka Tume ya Ulaya; mpokeaji wa Data ya Kibinafsi anapatikana Marekani na ametimiza masharti ya Mfumo wa Ulinzi wa Faragha wa Umoja wa Ulaya na Marekani; Paxful imeweka mbinu za ulinzi zinazofaa kuhusiana na utumaji huo, kwa mfano, kwa kuweka makubaliano ya Sheria za Kawaida za Mkataba za Umoja wa Ulaya na mpokeaji, au; sheria inayotumika inatoa hali ya kipekee inayopinga utumiaji wa GDPR kwa utumaji wa jumla. Ili upate nakala ya mbinu ambazo Paxful imeweka ili kusaidia katika michakato yake ya utumaji wa data ya kibinafsi nje ya EEA, wasiliana nasi jinsi ilivyoelezewa katika sehemu iliyo hapo juu ya “Wasiliana Nasi”.

Hati ya Nyongeza ya California

Ufumbuzi ufuatao unatumika kwa, na umekusudiwa hasa kwa, wakazi wa Jimbo la California.

Haki Zako za Faragha za California

Kwa kiwango ambapo tunafichua maelezo fulani yanayomtambulisha mtu binafsi yanayokuhusu kwa watu wengine ambao wanayatumia kwa madhumuni yao ya kukutumia matangazo moja kwa moja, una haki ya kuomba maelezo ya ziada kuhusu wapokeaji wa maelezo yako. Ili utumie haki hii, tafadhali wasiliana nasi jinsi ilivyobainishwa katika sehemu iliyo hapo juu ya “Wasiliana Nasi.”

Ufichuaji wa Kutofuatilia

Tovuti yetu haijabuniwa kushughulikia maombi au ishara za “Usifuatilie”.

Maelezo Paxful inazifanyia nini taarifa zako binafsi?
Kwa nini?

Kampuni za fedha huchagua jinsi ya kushiriki maelezo yako binafsi. Sheria ya nchi inawapa watumiaji haki ya kudhibiti kiwango fulani lakini sio ushiriki wote. Sheria ya nchi pia inasisitiza tukuambie jinsi tunavyokusanya, kushiriki, na kulinda maelezo yako binafsi. Tafadhali soma notisi hii kwa umakini ili uelewe tunachokifanya.

Nini?

Aina ya maelezo binafsi tunayokusanya na kushiriki inategemea bidhaa au huduma ulizonazo nasi. Maelezo haya yanaweza kujumuisha:

  • Namba ya Bima ya Jamii au masalio ya akaunti
  • Historia ya malipo au historia ya miamala
  • Historia ya mikopo au alama za mikopo

Pale unapoacha kuwa mteja wetu, tutaendelea kushiriki taarifa zako kama inavyoainishwa kwenye notisi hii.

Kwa jinsi gani?

Kampuni zote za fedha zinapaswa kushiriki maelezo binafsi ya wateja ili kuendesha biashara zao za kila siku. Katika sehemu iliyo hapa chini, tunaorodhesha sababu zinazofanya kampuni za biashara zishiriki maelezo binafsi ya wateja wake; sababu zinazofanya Paxful kushiriki; na iwapo unaweza kudhibiti ushiriki huu.


Sababu zinazoweza kufanya tushiriki taarifa zako binafsi

Je, Paxful inashiriki?

Unaweza kudhibiti ushiriki huu?

Kwa ajili ya malengo yetu ya kibiashara ya kila siku - kama kuchakata miamala yako, kuboresha akaunti yako/zako, kujibu maagizo ya mahakama na uchunguzi wa kisheria, au kuripoti kwa mamlaka za mikopo

Ndiyo

Hapana

Kwa ajili ya malengo yetu ya mauzo - ili kutoa bidhaa na huduma zetu kwako

Ndiyo

Hapana

Kwa ajili ya utangazaji masoko pamoja na kampuni zingine za kifedha

Ndiyo

Hapana

Kwa ajili ya malengo ya biashara ya kila siku ya washirika wetu - maelezo kuhusu miamala na hali ya huduma uliyopokea

Ndiyo

Hapana

Kwa ajili ya malengo ya biashara ya kila siku ya washirika wetu - maelezo kuhusu thamani yako ya kupokea mkopo

Hapana

Hatushiriki

Kwa wasio washirika kukuuzia

Hapana

Hatushiriki

Maswali?

Nenda kwenye www.paxful.com

Kutuhusu

Ni nani anatoa notisi hii?

Notisi ya faragha inatolewa na Paxful na inatumika kwa akaunti yako binafsi ya Paxful.

Tunachokifanya

Ni kwa jinsi gani Paxful inalinda taarifa zangu binafsi?

Ili kulinda maelezo yako binafsi dhidi ya ufikiaji na utumiaji usioidhinishwa, tunatumia njia za ulinzi ambazo zinafuata sheria za nchi. Njia hizi zinajumuisha ulinzi wa kompyuta na mafaili na majengo yanayolindwa.

Paxful hukusanya maelezo yangu binafsi kwa njia gani?

Tunakusanya maelezo yako binafsi, kwa mfano, pale ambapo

  • unafungua akaunti au kutoa maelezo ya akaunti
  • unatupatia maelezo ya mawasiliano au kutuma pesa
  • unapotumia akaunti yako ya Paxful kutuma au kupokea fedha

Pia tunakusanya maelezo binafsi kutoka kwa makundi mengine, kama taasisi za mikopo, washirika, na makampuni mengine.

Kwa nini siwezi kudhibiti ushiriki wote?

Sheria ya nchi inakupa haki ya kudhibiti tu

  • ushiriki kwa ajili ya malengo ya biashara ya kila siku ya washirika — maelezo kuhusu thamani yako ya kupokea mkopo
  • washirika wsitumie maelezo yao kukutangaza
  • ushiriki kwa wasio washirika kutangaza masoko kwako

Sheria za majimbo na makampuni binafsi zinaweza kukupa haki ya kudhibiti ushiriki. Angalia hapa chini kwa maelezo zaidi juu ya haki yako chini ya sheria ya jimbo.

Ufafanuzi

Washirika

Kampuni zinazohusiana kutokana na umiliki au udhibiti mmoja. Zinaweza kuwa kampuni za kifedha au zisizo za kifedha.

  • Washirika wetu ni pamoja na kampuni zilizo chini ya udhibiti wa Paxful Holdings, Inc.

Kampuni zisizo washirika

Kampuni zisizohusiana kutokana na umiliki au udhibiti mmoja. Zinaweza kuwa kampuni za kifedha au zisizo za kifedha.

  • Kampuni zisizo washirika tunaoshiriki nao maelezo binafsi zinazohusisha watoa huduma ambao wanatoa huduma au kufanya kazi kwa niaba yetu.

Uuzaji wa pamoja

Makubaliano rasmi kati ya kampuni za kifedha zisizo washirika ambazo kwa pamoja zinatangaza bidhaa na huduma za kifedha kwako.

  • Washirika wetu wa utangazaji masoko wa pamoja ni pamoja na kampuni za kifedha.

Maelezo mengine muhimu

Tunaweza kutuma maelezo binafsi kwenda nchi nyingine, kwa mfano, kwa ajili ya huduma ya wateja au kwa ajili ya kuchakata miamala.

California: Ikiwa akaunti yako ya Paxful ina anwani ya posta ya California, hatutashiriki maelezo yako binafsi tunazokusanya kukuhusu isipokuwa kwa kiwango kinachoruhusiwa chini ya sheria ya jimbo la California.

Vermont: Ikiwa akaunti yako ya Paxful ina anwani ya Vermont, hatutashiriki maeezo yako binafsi tunayokusanya kukuhusu kwa makampuni yasiyo washirika wetu isipokuwa kama sheria inaruhusu au wewe utatoa idhini.