Ukumbusho wa Vigezo vya Huduma vya Mchuuzi

Haya Masharti ya Huduma ya Mchuuzi yananuiwa kutumika kama rejeleo fupi la mchuuzi tu, na kwa namna yoyote hayachukui nafasi ya Masharti ya Huduma ya Paxful.

Tafadhali kumbuka kwamba unakubali vigezo vifuatavyo unapochagua kuchuuza kwenye Paxful.

 1. Kama mchuuzi, unapaswa kukubali hatari zote na kuwajibika kwa ulaghai wowote utakaokukabili wakati wa uuzaji wa mali zako za kidijitali.
 2. Paxful ina haki ya kutokurejeshea fedha zozote zilizopotea kutokana na ulaghai au malipo yaliyofanywa kwenye ada ya eskro yetu.
 3. Malipo yoyote ya kodi ni wajibu wa mchuuzi.
 4. Ili kuripoti tatizo kwenye uchuuzi, tafadhali fungua mashtaka na usubiri mpatanishi aingilie kati.
 5. Paxful haiwajibiki katika hali ambazo umeachilia mali za kidijitali kabla ya malipo kukamilika.
 6. Vitendo vifuatavyo haviruhusiwi kwenye Paxful na vinaweza kupelekea akaunti yako kufungiwa:
  1. Uuzaji tena wa kadi za zawadi
  2. Kushiriki maelezo ya eskro katika uchuuzi
  3. Kuchuuza bila kutumia eskro
  4. Kutojibu - wachuuzi wanatakiwa kujibu kwa haraka
  5. Lugha chafu
  6. Kumuiga mpatanishi
  7. Kuunda akaunti rudufu (bila ruhusa)
  8. Majadiliano
  9. Ufungaji wa sarafu wa makusudi
  10. Aina nyingine yoyote ya kitendo cha ulaghai