Tafadhali subiri ili tukutafutie ofa bora zaidi.

Uzia

Lipwa kwa kutumia

Bei kwa kila Tether

Jinsi ya Kuuza Tether kwenye Paxful

Hapa Paxful, tunasaidia watu kukaribia zaidi kupata uhuru wa kifedha na kujiajiri wenyewe. Hii ndiyo sababu mbali na Bitcoin, sasa unaweza kuuza Tether (USDT) moja kwa moja kwa zaidi ya watumiaji milioni tatu duniani kote. Kupitia malipo yanayolindwa na eskro, uhuru wa kuweka viwango vyako na zaidi ya njia za malipo 300 unazoweza kuchagua, soko letu linalowezeshwa na watu linafanya iwe rahisi sana kwa kila mtu kupata faida.

Ili kuanza, jiunge na Paxful au uingie kwenye akaunti iliyopo na ufuate hatua hizi:

  1. Weka muundo wa malipo unaopendelea na sarafu unayotaka itumike kukulipa.
  2. Bofya Tafuta Ofa ili kuangalia orodha ya ofa ambazo zinafikia masharti uliyoyaweka.
  3. Unapoangalia ofa, angalia maelezo yote kwa umakini. Hii ni pamoja na alama za sifa za mnunuzi, upatikanaji wao, na viwango vilivyopendekezwa. Ikiwa hauwezi kupata mlingano mzuri, unaweza ku unda ofa yako mwenyewe ili uvutie watumiaji ambao wanahitaji kununua Tether kwa vigezo vyako.
  4. Mara utakapopata ofa unayoipenda, bofya Uza. Haitaanzisha biashara; badala yake, utaweza kuona vigezo na masharti ya mnunuzi.
  5. Kama utakubaliana na vigezo, weka kiasi unachotaka kuchuuza na ubofye Uza Sasa. Hii itaanzisha biashara na kuhamisha USDT zako hadi kwenye mfumo wetu salama wa eskro.
  6. Zingatia maelekezo ya mnunuzi na utoe maelezo muhimu kwenye gumzo la moja kwa moja. Mara utakapopokea malipo, unaweza kuachilia USDT kutoka kwenye eskro yetu kwenda kwenye pochi ya mnunuzi, na kuhifadhi risiti iliyo wazi kwa umma.
  7. Baada ya biashara, mara zote kumbuka kuacha maoni juu ya mnunuzi. Hii siyo tu kwamba inamsaidia kujenga sifa zake, lakini pia inawawezesha wachuuzi wengine kujua wanajihusisha na nani.

Ili kuhakikisha ufanyaji wa biashara bila wasiwasi, soma kanuni zetu za kuuza Bitcoin na Tether. Unaweza pia kufuatilia mwongozo wetu wa kuunda vigezo vizuri vya ofa ili uweze kuunda ofa bora kwa wanunuzi wako.

Hapa Paxful, tumechukua hatua kali ili uweze kuchuuza kwa usalama wakati wote, mahali popote. Pitia maelfu ya ofa halali na uanze kuuza Tether leo!