Vigezo vya Huduma vya Paxful Earn

Tarehe ya kuanza: Julai 1, 2021

TAFADHALI SOMA MAKUBALIANO HAYA KWA MAKINI. Kwa kutumia huduma ya Paxful Earn, unakubali kujifunga na makubaliano haya ya "Vigezo vya Huduma vya Paxful Earn" na unatambua na kukubali kwamba umesoma kwa makini na kwa kina, umeelewa, na umekubali vigezo na masharti yote yanayojumuishwa humu, ambayo ni nyongeza ya Vigezo vya Huduma vya Paxful ("Makubaliano"). Vigezo vyovyote vilivyo katika herufi kubwa vilivyotumiwa lakini havijafafanuliwa hapa chini vina maana zilizoelezwa katika Makubaliano. Kama kukotokea mgogoro wowote kati ya Makubaliano na Vigezo vya Huduma vya Paxful Earn wakati wa au kuhusiana na matumizi yako ya huduma ya Paxful Earn, basi makubaliano ya Vigezo vya Huduma vya Paxful Earn yatatumiwa.

Kuhusu Paxful Earn

Huduma ya Paxful Earn iko katika mfumo wa ushirikishi unaokuruhusu wewe, mtumiaji uliyethibitishwa wa Paxful, kuhamisha Mali yako ya Kidijitali kwa jukwaa la mshirika ("Mshindani wa Earn"), ambapo unaweza kupata faida kwa kushikilia chagua Mali ya Kidijitali kwenye pochi zake.

Mfumo wa Ushirikishi

Huduma ya Paxful Earn ni mfumo wa ushirikishi unaopatikana kupitia mfumo wa Paxful. Kwa kuonyesha kuwa ungependa kushiriki katika Paxful Earn, unaipa Paxful idhini ya kushiriki maelezo ya akaunti yako ya Paxful na Mshindani wa Earn na maelezo ya kibinafsi yanayokutambulisha hasa kwa ajili ya kuwezesha Mshindani wa Earn kukadiria ustahiki wako wa kushiriki kwenye huduma ya Paxful Earn. Maelezo haya yanaweza kujumuisha, lakini sio tu, jina lako, siku ya kuzaliwa, na jimbo na nchi unamoishi. Mshindani wa Earn anaweza kuitisha maelezo ya ziada. Kwa hivyo ni lazima ufuate maelekezo yanayowekwa ili uwasilishe maelezo yoyote ya ziada. Mshindani wa Earn anaweza kuweka, kufikia, kuhamisha au kutumia maelezo yako ya binafsi kwa njia tofauti na yetu. Ikiwa hutaki kushiriki maelezo ya kibinafsi yanayokutambulisha na Mshindani wa Earn, basi usishiriki kwenye Paxful Earn.

Baada ya uthibitisho, unaweza kuchagua aina ya/za mali ya Kidijitali na zawadi zinazohusika zinazotolewa na Mshindani wa Earn kwa uwekaji. Mara baada ya kuweka Mali za kidijitali, Mali hizo za Kidijitali zitawekwa kwenye pochi yako ya Paxful na kuhamishwa kwenye jukwaa la Mshindani wa Earn. Mali ya Kidijitali iliyowekwa pamoja na faida iliyotokana nayo zinaweza kuonekana kupitia ukurasa wa Pochi Yangu / Earn kwenye jukwaa la Paxful.

The interest earned by Users is determined by, and subject to the rules of, the Earn Counterparty and may be changed or modified by the Earn Counterparty at its sole discretion. By entering into a transaction with the Earn Counterparty you agree to be bound by the Earn Counterparty’s Terms of Service. The Earn Counterparty Terms of Service are valid in all cases except when they contradict or violate the Agreement, these Paxful Earn Terms of Service, are illegal, are unreasonable or otherwise difficult to comply with (as determined in Paxful’s sole and absolute discretion), or if you and the Earn Counterparty consent to alter the Earn Counterparty Terms. IT IS YOUR RESPONSIBILITY TO CAREFULLY READ THE EARN COUNTERPARTY TERMS AND FOLLOW THEM EXACTLY. IF YOU DO NOT FOLLOW THE EARN COUNTERPARTY TERMS, YOUR TRANSACTION MAY BE DENIED. NEVER ENTER INTO A PAXFUL EARN SERVICE TRANSACTION UNLESS YOU HAVE FOLLOWED ALL TERMS AND CONDITIONS LISTED. IF YOU FAIL TO FOLLOW THE TERMS AND CONDITIONS, PAXFUL MAY NOT BE ABLE TO ASSIST YOU IN A DISPUTE PROCESS TO RECOVER YOUR FUNDS.

Ada

Paxful itakuwa wazi siku zote kuhusu ada zetu. Ada zozote zitatumika kwenye matumizi ya huduma za Paxful. Kwa maelezo zaidi na masasisho ya viwango vya ubadilishaji, tafadhali rejelea Kituo cha Msaada.

Akaunti Zinazostahili na Maeneo Yaliyo na Vizuizi

Huduma ya Paxful Earn inapatikana kwa watumiaji waliotimiza masharti ya huduma hio pekee. Paxful ina haki ya kuzuia au kubadilisha huduma ya Paxful Earn kwa mtumiaji yeyote wa Paxful, na Mpinzani wa Earn anaweza kukataa mauziano yoyote na mtumiaji yeyote wa Paxful. Pamoja na Maeneo yenye Vikwazo kama ilivyoelezwa katika Sehemu ya 2.7 ya Vigezo vya Huduma, huduma ya Paxful Earn haipatikani kwa watumiaji wanaoishi katika Jimbo la Texas, pamoja na nchi au jimbo lingine lolote lililowekewa vikwazo na vigezo vya huduma vya Mshindani wa Earn.

HAKUNA DHAMANA, KIMA CHA WAJIBU & KUKUBALI HATARI

HUDUMA ZA PAXFUL EARN ZINATOLEWA KATIKA MSINGI WA "KAMA ILIVYO" NA "KAMA INAVYOPATIKANA" BILA UDHAMINI, UWAKILISHI AU DHAMANA YOTOTE IWE NI KWA MAELEZO, MADOKEZO AU YA KISHERIA. KWA KIASI CHOTE KINACHORUHUSIWA NA SHERIA INAYOTUMIKA, PAXFUL INAKANUSHA UDHAMINI WOWOTE WA CHEO, UCHUUZI, UKAKAMAVU KWA KUSUDI MAALUM NA/AU UKIUKAJI. PAXFUL HAIFANYI UWAKILISHI WOWOTE AU UDHAMINI UNAOFIKIA TOVUTI, SEHEMU YOYOTE YA HUDUMA, NYARAKA ZOZOTE ZILIZOJUMUISHWA HAPA, ZITAKUWA ENDELEVU, ZISIZOINGILIWA, KWA WAKATI, AU ZISIZO NA DOSARI. PAXFUL HAITAWAJIBIKA KWA KUSHINDWA KWA PROGRAMU AU TEKNOLOJIA YA MSHIRIKA, USUMBUFU WOWOTE AU UPOTEVU ANAOWEZA KUKUMBANA NAO MTUMIAJI. UNATAMBUA NA KUKUBALI KWAMBA HUJATEGEMEA KAULI AU UELEWA MWINGINE, UWE WA MAANDISHI AU WA MDOMO, KUHUSIANA NA MATUMIZI YAKO YA HUDUMA NA TOVUTI. PASIPO KUWEKA KIMA CHA MWENDELEZO UNATAMBUA NA KUKUBALI HATARI ZOZOTE ZINAZOTOKANA NA KUTUMIA SARAFU ZA KIDIJITALI IKIJUMUISHA HATARI ZA KISHERIA, HITILAFU ZA NYENZO, MATATIZO YA PROGRAMU, KUSHINDWA KUUNGANISHA MTANDAO WA INTANETI, PROGRAMU ZISIZO SALAMA, MUINGILIANO WA MSHIRIKA MEINGINE, UNAOPELEKEA UPOTEVU AU KUSHINDWA KUFIKIA AKAUNTI AU POCHI YAKO NA DATA ZINGINE ZA MTUMIAJI, KUSHINDWA KWA SEVA AU UPOTEVU WA DATA. UNAKUBALI NA KUTAMBUA KWAMBA PAXFUL HAITAWAJIBIKA KWA KUSHINDIKANA KWA MUUNGANISHO, UVURUGAJI, HITILAFU, UHARIBIFU AU UCHELEWESHAJI UNAOWEZA KUKABILIANA NAO UNAPOTUMIA HUDUMA,VYOVYOTE UNAVYOWEZA KUSABABISHWA.

PAXFUL, WASHIRIKA NA WATOA HUDUMA WAKE, AU MAOFISA, WAKURUGENZI, MAWAKALA, WAFANYAKAZI, WASHAURI AU WAWAKILISHI, KWA NAMNA YOYOTE HAWATAWAJIBIKA KWA (A) KIASI CHOCHOTE KILICHO KIKUBWA KULIKO THAMANI YA JUMLA YA ADA INAYOLIPWA NA WEWE KWA AJILI YA HUDUMA AMBAYO INATOLEWA KATIKA MIEZI KUMI NA MBILI (12) KABLA YA KUTOKEA KWA UPOTEVU (B) KWA FAIDA YOYOTE ILIYOPOTEA, KUPUNGUA THAMANI AU FURSA YA BIASHARA, UPOTEVU, UHARIBIFU WOWOTE, RUSHWA AU UVUJAJI WA DATA AU MALI NYINGINE YOYOTE ISIYOSHIKIKA AU UHARIBIFU WOWOTE WA BAHATI MBAYA, USIO WA MOJA KWA MOJA, USIOSHIKIKA, AU WA MATOKEO YA MADHARA, IWE NI KULINGANA NA MKATABA, UHARIBIFU, UZEMBE, WAJIBU, AU UNAOTOKANA NA AU KULINGANA NA MATUMIZI YALIYOIDHINISHWA AU YASIYOIDHINISHWA YA WAVUTI AU HUDUMA, AU MAKUBALIANO HAYA, HATA KAMA MWAKILISHI WA PAXFUL ALIYEIDHINISHWA AMESHAURIWA AU ALIJUA AU ALIPASWA KUJUA UWEZEKANO WA UHARIBIFU HUO, NA PAMOJA NA HAYO KUSHINDWA KWA TIBA ILIYOKUBALIWA AU NYINGINE KWA KUSUDI LAKE, ISIPOKUWA KWA KIASI CHA HUKUMU YA MAHAKAMA AMBACHO UHARIBIFU HUO ULIKUWA MATOKEO YA UZEMBE WA PAXFUL, UDANGANYIFU, UTOVU WA NIDHAMU AU UKIUKAJI WA KUKUSUDIA WA SHERIA. BAADHI YA MAMLAKA HAZIRUHUSU UONDOLEWAJI AU KIMA CHA UHARIBIFU WA BAHATI MBAYA AU KUTOKUSUDIA, HIVYO KIMA CHA HAPO JUU VINAWEZA VISIKUHUSU WEWE.

Unakiri na kukubali kuwa Paxful inajisimamia kama mtoa huduma wa jukwaa la huduma hii ya Paxful earn. Pia unakubali kuwa Paxful haitadhibiti wala haitawajibika kwa mipango ya msingi inayoleta faida ya Mshindani wa Earn. Paxful haitawajibika kwa hasara zozote zitakazotokana na matatizo ya mikataba mahiri, matukio ya kuingia kwenye akaunti bila idhini wala kusimamisha kwa muda, kutoendeleza matumizi au kukatizwa kwa biashara, kufilisika, kufungwa kwa muda kusio kwa kawaida au kusimamishwa kwa uuzaji wa Mshindani wa Earn au matatizo mengine ambayo huenda yakatokea. Unakubali kushughulikia hatari zote zinazohusishwa na jukwaa la Mshindani wa Earn na hasara zote ambazo zinaweza kutokana na hatari zilizotajwa hapo juu. Ukipata hasara yoyte kutokana na hatari zilizotajwa hapo juu, unakubali kuwa sehemu sawia ya pesa zako zilizowekwa kando ulizopoteza kwenye akaunti yako zitatumika kulingana na kiwango cha uharibifu au hasara.

Unakubali kuwa iwapo sehemu yoyote ya huduma ya Paxful Earn iliyotolewa na Paxful au Mshindani wa Earn hazifikiwi au zinakatizwa kutokana na hali hii, Paxful haitawajibika kwa hasara yako au ya mtu mwingine (ikiwa ni pamoja na lakini sio tu hasara yoyote ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja) inayoweza kutokana na shughuli hiyo:

  1. Kusimamishwa kwa muda, kutoendelezwa, kufungwa au kukatizwa kabisa kwa biashara ya Mshindani wa Earn;
  2. Kusimamisha huduma kwa muda kwa ajili ya matengenezo kama ilivyotangazwa na Mshindani wa Earn au Paxful;
  3. Hitilafu ya mfumo wakati wa kusafirisha data;
  4. Hali isiyotarajiwa au ajali nyingine inayotokana na sababu ambazo hazikutarajiwa, zisizoepukika au zisizo na suluhisho kama vile kimbunga, mtetemeko wa ardhi, sunami, mafuriko, baa, kukatizwa kwa umeme, vita, msukosuko, hatua za serikali, mashambulizi ya kigaidi, n.k, yanayosababisha kusimamishwa kwa muda kwa jukwaa za Paxful au Mshindani wa Earn;
  5. Hitilafu ya huduma, kukatizwa au kucheleweshwa kunakotokana na udukuzi, virusi kwenye kompyuta, mabadiliko au hiitilafu ya kiufundi, uboreshaji wa tovuti, matatizo ya benki au kufungwa kwa muda kutokana na sheria za serikali;
  6. Hitilafu ya huduma, kukatizwa, kucheleweshwa, ukosefu wa mwitikio wa mfumo, au mwitikio uliocheleweshwa wa mfumo unaotokana na kuharibika, kutokea kwa hitilafu au vinginevyo kutoweza kufanya kazi kama kawaida kwa mfumo wa kompyuta wa jukwaa la Mshindani wa Earn au Paxful;
  7. Matatizo ya kiufundi yasiyo ya kawaida ambayo hayawezi kutabiriwa wala kusuluhishwa na mbinu za kiufundi zilizo kwenye sekta;
  8. Makosa au kuchelewa kwa watu wengine; au
  9. Mabadiliko katika sheria zozote zinazotumika, kanuni au maagizo ya serikali.

Pia unakubali kuwa kutokea kwa hali iliyotajwa hapo juu kunaweza kusababisha mauziano yasiyo ya kawaida, kukatizwa kwa shughuli za soko na matukio mengine ambayo huenda si ya kawaida na Paxful ina haki ya kukataa kuchakata mauziano yako wakati wowote.