Tafadhali subiri ili tukutafutie ofa bora zaidi.

Nunua kutoka

Lipa kwa

Bei kwa kila Bitcoin

Jinsi ya Kununua Bitcoin kwa kutumia Venmo

Kama unataka kununua Bitcoin lakini hauna njia nyingine ya kutuma fedha au hauna mashaka kuhusu faragha, Venmo ni njia bora zaidi ya malipo kwa ajili yako. Ni rahisi kutumia - unatakiwa tu kupakua programu na kuunganisha akaunti ya benki yako na akaunti yako ya Venmo.

Ili kununua BTC kwa kutumia Venmo, kwanza unatakiwa kujiunga na pochi ya Bitcoin bila malipo kwa kubofya kitufe cha Fungua akaunti. Pia utatakiwa kuthibitisha utambulisho wako kwetu kabla ya kununua BTC.

Baada ya kuingia kwenye akaunti, bofya kitufe cha Nunua Bitcoin na uchague Venmo kama njia ya malipo ili kuchuja ofa zisizostahili. Tunapendekeza ukague wasifu wa muuzaji ili kupima uaminifu wao kwa kubofya kwenye jina lake ili kuona historia yake ya uchuuzi na maoni kutoka kwa washirika wa biashara waliopita.

Chagua ofa unayoipenda zaidi na ubofye kitufe cha Nunua ili kuangalia masharti ya uchuuzi na uanze kufanya uchuuzi. Kuwa tayari kuchapisha picha ya kujipiga ukiwa umeshika Kitambulisho halali au picha ya skrini ya akaunti yako ya Venmo pale utakapoulizwa na muuzaji. Pesa zako zimelindwa katika hatua hii na eskro ya Paxful ambapo Bitcoin za muuzaji zimetengwa kwa muda hadi hapo uchuuzi utakapokamilika au kughairiwa.

Bofya kitufe cha Tia Alama kuwa Imelipwa mara tu utakapotuma pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Venmo na kumsubiri muuzaji aachilie Bitcoin zako kutoka kwenye eskro kwenda kwenye pochi yako ya Paxful. Ni hivyo tu! Pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Venmo sasa zimekuwa Bitcoin.

Kama una maoni kuhusu soko letu au unataka kufungua shtaka, kuwa huru kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi wa wateja. Tuko mtandaoni wakati wote, siku yoyote ya wiki ili kukusaidia juu ya hitaji lako.