Kutana na timu ya Paxful!

Wafanyakazi wa Paxful ni moyo wa kampuni. Wenye tamaduni na historia tofauti, mara zote tunajifunza kutoka kwa kila mmoja kati yetu. Sehemu nzuri zaidi ni ipi? Kila mmoja anaweza kujifunza lugha na tamaduni tofauti. Tunaweza kuwa na timu inayoshughulikia bidhaa lakini jukwaa letu ni matokeo ya kazi shirikishi na maoni kutoka kwa kila timu na idara.

Max

Ushauri wa Kibiashara (Marekani)

Ni kitu gani ambacho huwezi kukaa siku moja bila kukifanya hapa Paxful?

Kutaniana na wafanyakazi wenzangu.

Nini kinakupa motisha hapa Paxful?

Uwezekano wa kufanikiwa. Kampuni hii ina uwezekano mkubwa wa kufanikiwa, na ninafahamu kwamba ninaweza kuchangia sehemu kubwa ili tukifikia mafanikio hayo.

Ni kitu gani kimoja kuhusu Paxful/huduma ya fedha ya mtu kwa mtu ambayo unatamani kila mmoja angeifahamu?

Watu huuliza kwa nini huduma ya fedha ya mtu kwa mtu ni muhimu. Benki ya Dunia ilithibitisha kwamba takribani watu bilioni 2 hawawezi kufikiwa na huduma za kawaida za kifedha. Paxful inawapa watu hao fursa ya kujumuika katika mfumo wa kifedha.

Lana

Afisa Mkuu wa Usimamizi wa Sheria (Marekani)

Nini kinakupa motisha hapa Paxful?

Msukumo na nguvu chanya ya kuileta Bitcoin kwa watu.

Je, ni athari gani yenye maana sana kuhusu kazi yako?

Nina mamlaka ya kuhakikisha kwamba tunawakamata watu wabaya. Nimeipatia timu yangu nyenzo na taratibu za kufanya hivyo. Hatuna uvumilivu na ulaghai na vitendo viovu kwenye wavuti.

Trisha

Mwelekezaji wa kidijitali (Ufilipino)

Ni manufaa gani mazuri zaidi hapa Paxful?

Ninapenda manufaa ya kwenda kwenye chumba cha mazoezi na eneo la kukandwa mwili! Hakika Kampuni inajali afya ya wafanyakazi wake na marupurupu haya yanakusaidia kupata muda wa mapumziko wakati unakumbwa na msongo sana.

Ni kitu gani kimoja kuhusu Paxful/huduma ya fedha ya mtu kwa mtu ambayo unatamani kila mmoja angeifahamu?

Ningependa watu wafahamu zaidi kuhusu sekta hii kwa ujumla. Sekta ya fedha ya mtu kwa mtu ina faida nyingi sana, hasa kwa wasiotumia benki.

Je, ni hafla gani ya kampuni ya Paxful unayoipendelea zaidi ambayo umeshahudhuria?

Je, ni hafla gani ya kampuni ya Paxful unayoipendelea zaidi ambayo umeshahudhuria?

Ysabelle

Mauzo kwa Njia ya Video (Ufilipino)

Nini kinakupa motisha hapa Paxful?

Kinachonifanya niendelee ni fursa za ukuaji zisizo na kikomo mahali hapa. Hata pale nilipokuwa mdogo, waliniamini mimi na kazi yangu. Walinipa nafasi ya kuonyesha ninachoweza kufanya.

Je, ni hafla gani ya kampuni ya Paxful unayoipendelea zaidi ambayo umeshahudhuria?

Kila wakati tunapotoka kupata vinywaji, ni wakati wa furaha sana na njia nzuri kwangu kuimarisha ukaribu na wenzangu nje ya muda wa kazi!

Je, ni athari gani yenye maana sana kuhusu kazi yako?

Kazi yangu inaniruhusu kubadili shauku yangu kuwa kazi inayoleta athari bora kwa wale wanaotazama video tunazotengeneza.

Michelle

Mchambuzi wa Ubora wa Maoni (Ufilipino)

Ni manufaa gani mazuri zaidi hapa Paxful?

Seeing the whole team improve, working at our best with genuine smiles on our faces. Being a part of that process for improvement keeps my drive going here at Paxful. And of course when the value of Bitcoin rises!

Ni kitu gani kimoja kuhusu Paxful/huduma ya fedha ya mtu kwa mtu ambayo unatamani kila mmoja angeifahamu?

Ninataka kila mmoja awe na ufahamu sahihi juu ya jinsi Bitcoin inavyofanya kazi kwa ujumla na jinsi mchakato wa uchuuzi unavyofanya kazi hapa paxful ili waweze kuelewa vizuri iwapo wanatapeliwa au la.

Ni kitu gani ungependa kuona Paxful ikikifanikisha au kukifanya kama kampuni katika miaka michache ijayo?

Kuwa kampuni ya kwanza ya teknolojia ya fedha na jukwaa la uchuuzi la mtu kwa mtu!

Madis

Msanidi wa PHP (Estonia)

Ni kitu gani ambacho huwezi kukaa siku moja bila kukifanya hapa Paxful?

Kutafuna matunda na karanga jikoni, hasa korosho.

Nini kinakupa motisha hapa Paxful?

Watu ninaofanya nao kazi na malengo ya kampuni yanayosaidia watu kufikia huduma za kifedha ambazo wasingeweza kuzifikia.

Ni kitu gani kimoja kuhusu Paxful/huduma ya fedha ya mtu kwa mtu ambayo unatamani kila mmoja angeifahamu?

Kwamba kuna njia halisi, zenye faida za kupata pesa kwenye Paxful na kwamba si kila mtu ni tapeli.

Pavel

Mhandisi wa Kubernetes (Estonia)

Ni kitu gani ambacho huwezi kukaa siku moja bila kukifanya hapa Paxful?

Kupata kahawa na wenzangu. Ni muda mzuri wa kupata maoni kutoka kwa yeyote na kujifunza kile kinachoendelea ndani ya idara zingine. Mazungumzo yasiyo rasmi yanaweza kuokoa masaa yanayotumiwa kwa vikao.

Ni manufaa gani mazuri zaidi hapa Paxful?

Kwenda kwenye mazoezi ya viungo, chakula cha mchana, siku za mapumziko. Hata hivyo, jambo la muhimu ambalo mara nyingi husahaulika, ni kwamba Paxful ni kampuni yenye uaminifu zaidi ambayo nimewahi kufanya nayo kazi maishani mwangu. Wanafanya kila wanaloweza kuifanya siku yako kuwa yenye furaha zaidi na kukufanya ujisikie kuwa ni wa muhimu.

Je, ni hafla gani ya kampuni ya Paxful unayoipendelea zaidi ambayo umeshahudhuria?

Hafla zuri zaidi lilikuwa ni Siku zetu za Majira ya Joto, ambapo kampuni nzima, ikijumuisha kila mtu kutoka ofisi zingine, tulikusanyika pamoja kwa ajili ya safari ya kujenga ushirikiano huko Split, Croatia. Ilikuwa ni wakati mzuri sana kukutana na wafanyakazi wenzangu, kufahamiana na kila mtu, na kujenga uhusiano halisi wa ushirikiano.

Aska

Msimamizi wa Sheria (Hong Kong)

Nini kinakupa motisha hapa Paxful?

Matokeo na wanakikundi wenzangu.

Ni kitu gani kimoja kuhusu Paxful/huduma ya fedha ya mtu kwa mtu ambayo unatamani kila mmoja angeifahamu?

Kwamba tunajaribu kila tuwezalo kuwalinda wauzaji na wanunuzi! Hatutaki kabisa kushikilia BTC zako.

Je, ni hafla gani ya kampuni ya Paxful unayoipendelea zaidi ambayo umeshahudhuria?

Kusafiri kwenda ofisi zingine kwa ajili ya ziara na mafunzo.

Tugba

Meneja wa Ushirika (Estonia)

Ni kitu gani ambacho huwezi kukaa siku moja bila kukifanya hapa Paxful?

Timu yangu!

Nini kinakupa motisha hapa Paxful?

Kuna fursa nzuri sana ya ukuaji katika mbinu zote za kitaalamu na usimamizi.

Ni kitu gani kimoja kuhusu Paxful/huduma ya fedha ya mtu kwa mtu ambayo unatamani kila mmoja angeifahamu?

Matukio yote ya Paxful yanafurahisha! Lakini nilipenda hasa Siku za Majira ya Joto ya 2019, ambapo tulimaliza wiki nzima huko Croatia.