Tafadhali subiri ili tukutafutie ofa bora zaidi.

Nunua kutoka

Lipa kwa

Bei kwa kila Tether

Jinsi ya kununua Tether kwenye Paxful

Paxful inadhamiria kufanya huduma za kifedha zifikiwe kwa mamilioni ya watu ambao hawafikiwi na benki duniani kote. Tunakupa uhuru wa kubadili fedha zako kwa Tether (USDT) na kuzitumia upendavyo; iwe ni kwa kulipia bidhaa na huduma, kulinda mali yako dhidi ya mfumuko wa thamani ya fedha, kununua sarafu za kidijitali, au kukinga dhidi ya kubadilika kwa thamani ya sarafufichwa.

Kwenye soko la Paxful linalotokana na nguvu ya watu, unaweza kununua Tether moja kwa moja kutoka kwa watumiaji wenzako duniani kote. Hakuna mabenki, mashirika, au viunganishi vingine vinavyohusishwa.

Unaweza kuanza hivi:

  1. Fungua akaunti au uingie kwenye akaunti iliyopo. Ukijisajili kwenye Paxful utapata pochi bila malipo ambapo unaweza kuhifadhi USDT zako.
  2. Chagua njia ya malipo, weka kiasi unachotaka kutumia kwenye sarafu unayopendelea, kisha ubofye Tafuta Ofa.
  3. Pitia kila ofa na ukague vigezo na masharti yake. Kuwa mwangalifu kwa viwango vilivyowekwa na wauzaji, pamoja na alama za sifa zao na maoni ili kupima uaminifu wao.
  4. Mara utakapopata ofa inayotimiza masharti yako, thibitisha kiasi utakacholipa na uanze biashara. Hii itafungua gumzo la moja kwa moja ambapo unaweza kuwasiliana na muuzaji wakati huo huo.
  5. Wakati wa biashara, muuzaji atatoa maelezo zaidi juu ya jinsi ya kuendelea. Fuata maelekezo yake kwa umakini na uthibitishe muamala baada ya kufanya malipo.
  6. Mara baada ya muuzaji kuthibitisha malipo, ataachilia USDT zako zilizotunzwa salama kwenye eskro yetu, moja kwa moja kwenda kwenye pochi yako ya Tether ya Paxful.

Mara utakapomaliza biashara, unaweza kutumia salio lako la Tether kwa chochote upendacho, au kulituma hadi kwenye pochi nyingine.

Kupitia zaidi ya njia 300 za kulipa zinazojumuisha pesa taslimu, utumaji fedha kwa benki na kadi za zawadi, kununua USDT sasa ni rahisi mno. Je, huoni njia ya malipo unayopendelea? Tutaarifu na tutajaribu kuiongeza kwenye jukwaa letu. Kwa maelezo zaidi, angalia Hifadhi yetu ya Maelezo au uwasiliane na timu yetu ya usaidizi.