Tafadhali subiri ili tukutafutie ofa bora zaidi.

Nunua kutoka

Lipa kwa

Bei kwa kila Bitcoin

Jinsi ya Kununua Bitcoin kwa kutumia PayPal

PayPal ni moja ya mifumo ya utumaji fedha mtandaoni inayoongoza duniani na inafanya kazi kama mbadala wa hundi na maagizo ya pesa. Inatoa njia rahisi na ya haraka ya kutuma na kupokea fedha duniani kote, pamoja na kuchakata malipo wakati wowote, mahali popote.

Kununua Bitcoin kwa kutumia PayPal kwa haraka sasa inawezekana kwenye soko la mtu kwa mtu la Paxful. Unaweza kupata ofa mbalimbali zinazokubali PayPal kama njia inayopendelewa ya malipo kwenye jukwaa letu. Ikiwa hutapata ofa inayokufaa, unaweza kuunda ofa yako mwenyewe ili kuwavutia watumiaji wanaotaka kuchuuza BTC kwa kutumia PayPal.

Kwa ajili ya matumizi salama zaidi ya uchuuzi, baadhi ya wauzaji wanaweza kuhitaji hatua za ziada za kuthibitisha utambulisho wa washirika wao wa biashara. Hatua hizi zinaweza kukuhitaji kuwasilisha baadhi ya hati kama vile kadi za Vitambulisho, picha za kujipiga, na/au picha za skrini. Hii inapunguza hatari ya malipo ya kitapeli na matumizi yasiyohalalishwa ya akaunti za PayPal, na hivyo kuifanya Paxful kuwa soko salama zaidi.

Vigezo na mashati ya ofa vinaweza kutofautiana kidogo baina ya ofa moja na nyingine, hivyo hakikisha unasoma na kukubaliana na masharti ya muuzaji kabla ya kuanza uchuuzi. Unaweza kutumia Kikokotoo chetu cha Bitcoin cha mtandaoni ili kupata makisio ya kiasi cha BTC unachoweza kununua kwa kiasi cha sarafu ulichonacho. Kwa maelezo zaidi, unaweza pia kuangalia mwongozo wetu wa video wenye maelezo ya kutosha ya jinsi ya kununua Bitcoin kwa kutumia PayPal kwenye Paxful.

Hapa Paxful, tunakusudia kurahisisha namna unavyobadili fedha zako za PayPal kwenda Bitcoin kwa kutumia soko letu lililo salama na rahisi kutumia. Tafuta ofa inayokufaa zaidi leo.