Tafadhali subiri ili tukutafutie ofa bora zaidi.

Nunua kutoka

Lipa kwa

Bei kwa kila Bitcoin

Jinsi ya Kununua Bitcoin kwa kutumia Programu ya Cash

Cash App ni pochi ya mtandaoni na programu ya malipo ambayo inakuwezesha kutuma na kupokea pesa haraka kwa wanafamilia na marafiki. Pia inakuwezesha kukubali malipo kwa njia ya simu na kadi yanayolipwa kwa biashara yako na kutuma pesa kwenda kwenye akaunti yako ya benki.

Kwenye soko la mtu kwa mtu la Paxful, sasa unaweza kununua Bitcoin kwa kutumia Cash App. Fuata hatua hizi ili kupata BTC yako:

  1. Ingia kwenye akaunti ya Paxful – Ingia kwenye akaunti yako ya Paxful au fungua akaunti mpya. Kujisajili kwenye Paxful kunakupatia udhibiti wa pochi yako ya Bitcoin bila gharama yoyote ya ziada.
  2. Chagua njia yako ya malipo – Chagua Cash App kama njia ya malipo ili kupata orodha ya ofa zote zinazokubali njia hii ya malipo. Unaweza pia kuweka kiasi ulicho tayari kutumia ili kuchuja ofa zisizohitajika. Je, unataka kujua kiasi cha Bitcoin utakachokipata? Jaribu Kikokotoo chetu cha Bitcoin.
  3. Tafuta ofa nzuri – Pitia orodha ya ofa na uhakikishe unafanya ukaguzi wa awali. Zingatia upatikanaji, alama za sifa, historia ya uchuuzi wa muuzaji, na vitu vingine. Pindi utakapopata ofa nzuri inayokuridhisha, kagua vigezo vya mchuuzi kwa umakini kabla ya kuanza uchuuzi.
  4. Kubali vigezo na uanze uchuuzi – Unaponunua Bitcoin kwa kutumia Cash App, tayarisha $Cashtag yako na uthibitisho wa malipo kila mara ili kuwezesha mauziano rahisi. Baadhi ya wachuuzi wanaweza pia kukutaka uwasilishe nakala ya kadi ya Kitambulisho chako na hati nyingine ili kuthibitisha utambulisho wako. Hivyo jiandae kwa maombi kama hayo. Mara biashara itakapoanza, fuata maelekezo ya mchuuzi. Kumbuka kwamba Paxful inatumia mfumo wa eskro unaotenga Bitcoin za muuzaji hadi hapo muamala unapokamilika ili kukulinda dhidi ya utapeli utakaoweza kujitokeza. Mara biashara inapokamilika, utapokea Bitcoin moja kwa moja kwenye pochi yako ya Paxful.

Hapa Paxful, tunafanya iwe rahisi na salama kununua BTC kwa kutumia Cash App. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu namna ya kununua Bitcoin kwenye jukwaa letu, kuwa huru kuangalia msingi wetu wa maelezo au wasiliana na timu yetu ya usaidizi.