Sera ya Zawadi ya Kuripoti Hitilafu
Paxful, Inc. (inayorejelewa pia kama “Paxful,” “sisi,” “nasi,” au “yetu”) huchukua hatua za kuboresha bidhaa yetu na kutoa huduma salama kwa wateja wetu. Kwenye Sera hii ya Zawadi ya Kuripoti Hitilafu (“Sera”), tunaelezea hali zinazotumika kwa Mpango wetu wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu na jinsi unavyopaswa kutumiwa kuhusiana na matumizi yako ya tovuti yetu katika https://paxful.com/, ikiwa ni pamoja na, wala si, Pochi ya Paxful, mfumo wa mtandaoni wa biashara ya Bitcoin, programu ya kifaa cha mkononi, kurasa za mitandao ya kijamii au mali nyingine za mtandaoni (kwa ujumla, “Tovuti”), au unapotumia bidhaa, huduma, maudhui, vipengele, teknolojia au utendakazi wowote tunaotoa (kwa ujumla, “Huduma”). Sera hii imebuniwa ili kukusaidia upate maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kushiriki kwenye Mpango wetu wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu, matokeo salama ya utafutaji yanayotumika na manufaa unayoweza kupokea. Tafadhali kumbuka kuwa Huduma zetu tunazotoa zinaweza kutofautiana kulingana na eneo.
Kwa madhumuni yote, toleo la lugha ya Kiingereza la sera hii ya zawadi ya kuripoti hitilafu litakuwa zana halisi ya usimamizi. Ikiwa kutakuwa na tofauti yoyote kati ya toleo la lugha ya Kiingereza la sera hii ya zawadi ya kuripoti hitilafu na tafsiri yoyote itakayofuata kwa lugha nyingine yoyote, toleo la lugha ya Kiingereza litatumika.
Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu ni nini?
Ili kuboresha Paxful na Huduma, Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu wa Paxful unawapa watumiaji wetu fursa ya kujishindia zawadi kwa kutambua matatizo ya kiufundi.
Unawezaje kutueleza kuhusu matokeo yako ya Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu?
Mawasiliano yote kama hayo yanapaswa kuelekezwa kwa [email protected]. Kwenye mawasilisho yako, tafadhali bainisha maelezo kamili ya hitilafu na ushahidi unaoweza kuthibitishwa kuwa hitilafu hiyo ipo (ufafanuzi / hatua za kuthibitisha / picha za skrini / video / maandishi au nyenzo nyingine kama hizo).
Kanuni za Mpango
Ukiukaji wa mojawapo ya kanuni hizi unaweza kusababisha ukose kustahiki kupokea zawadi.
- Jaribu hitilafu kwenye akaunti unayomiliki tu au kwenye akaunti ambazo umeruhusiwa na mmiliki wa akaunti ili ufanyie jaribio hapo.
- Usiwahi kamwe kutumia matokeo ili kuhatarisha/kudukua data au kudukua mifumo mingine. Tumia ushahidi wa ukweli pekee ili kuonyesha tatizo.
- Ikiwa maelezo nyeti kama vile maelezo ya kibinafsi, vitambulisho, n.k.. yatafikiwa kama sehemu ya hitilafu, hayapaswi kuhifadhiwa, kuhamishwa, kufikiwa au kuchakatwa baada ya ugunduzi wa kwanza.
- Watafiti hawapaswi, na hawaruhusiwi kujihusisha kwenye shughuli yoyote ambayo inaweza kukatiza, kuharibu au kudhuru huduma ya Paxful.
- Watafiti hawapaswi kufichua hadharani hitilafu (kushiriki maelezo yoyote na mtu yeyote kando na wafanyakazi walioidhinishwa wa Paxful), au kushiriki hitilafu na mtu mwingine, bila ruhusa ya moja kwa moja ya Paxful.
Tunatathmini vipi matatizo yaliyotambuliwa chini ya Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu?
Matokeo yote hutathminiwa kwa kutumia mbinu inayolingana na kiwango cha hatari.
Mkataba wa Kutofichua Siri
Kabla hatujaanza kuzungumzia maelezo yoyote yanayohusiana na matatizo yaliyothibitishwa ambayo umetambua chini ya Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu, ikiwa ni pamoja na fidia, n.k., utahitaji kuweka Mkataba wa Kutofichua Siri nasi.
Tunalipa vipi zawadi za Mpango wa Kuripoti Hitilafu?
Zawadi zote kama hizo hulipwa na Paxful. Zawadi zote zinaweza kulipwa ikiwa tu hazikiuki kanuni na sheria zinazotumika, ikiwa ni pamoja na, wala si tu vikwazo na vizuizi vya kibiashara.
Tutachukua muda gani kuchanganua matokeo yako ya Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu?
Kutokana na hali ya utofauti na ugumu wa matatizo ya kiufundi, hatujaweka vipindi mahususi vya muda wa kuchanganua matokeo ya Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu. Uchanganuzi wetu hukamilika tu tunapothibitisha kuwepo kwa au kutokuwepo kwa hitilafu.
Ni hali gani ambazo hazijumuishwi kwenye Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu?
Hitilafu fulani zinazingatiwa kuwa hazishughulikiwi na Mpango wa Zawadi ya Kuripoti Hitilafu. Hitilafu hizo ambazo hazishughulikiwi ni pamoja na, wala si tu:
- Taka;
- Hitilafu za wizi wa data binafsi/kuhadaa watu;
- Mashambulizi ya DDOS;
- Matatizo ya kubuni ambayo hayana athari yoyote halisi;
- Hitilafu za usalama kwenye programu za watu wengine na kwenye tovuti za watu wengine zilizounganishwa na Paxful;
- Data ya kichanganuzi au ripoti zilizotengenezwa na kichanganuzi;
- Matatizo yaliyopatikana kupitia majaribio ya kiotomatiki;
- Hitilafu zilizochapishwa kwa umma kwenye programu ya Intaneti katika kipindi cha siku 30 baada ya kufichuliwa;
- Mashambulizi ya Udukuzi;
- Mashambulizi ya kuweka kichwa cha uongo cha mpangishaji yasiyo na athari mahususi inayoweza kuthibitishwa;
- Mashambulizi ya Self-XSS, ambayo ni pamoja na data ya ujumbe unaokusudiwa iliyowekwa na mwathiriwa;
- CSRF ya Kuingia/Kuondoka;
Maelezo Zaidi
Ikiwa unatafuta maelezo zaidi kuhusu Sera hii, unaweza kuwasiliana nasi kwa kutuma barua pepe kwa [email protected].