Sera ya AML

Paxful, Inc. na Paxful USA, Inc. (kibinafsi na kwa ujumla, “Kampuni”), iliyoanzishwa chini ya sheria za Jimbo la Delaware hutoa huduma kupitia soko la mtandaoni la mtu kwa mtu (“P2P”) kwa ununuzi na uuzaji wa mali dijitali.

Kampuni imesajiliwa kama Biashara ya Huduma za Pesa na shirika la United States Treasury Department’s Financial Crimes Enforcement Network (“FinCEN”). Sera na taratibu za Paxful za Kupinga Ulanguzi wa Pesa (“AML”) zimebuniwa ili kuzuia shughuli haramu kwenye mfumo, kulinda watumiaji, biashara na sarafu dijitali na jumuiya za huduma za fedha dhidi ya kulaghaiwa na wahalifu. Kampuni inatimiza masharti ya Sheria ya Siri ya Benki na mwongozo na kanuni zinazohusiana za FinCEN.

Kama sehemu ya sera za Utiifu za Paxful, sera na taratibu za Jua Mteja Wako (“KYC”) kwa wateja wa kibinafsi na wa taasisi zimebuniwa ili kuwezesha Kampuni kutengeneza imani thabiti kuwa inajua utambulisho halisi wa wateja wake ambao wamefanyiwa ukaguzi kama huo. Sera inatumika kwa watumiaji wote kwenye mfumo na inafuatwa na wafanyakazi, washauri, maofisa, wamiliki na wakurugenzi wote wa Kampuni.

Kupitia hatua ya kutumia mbinu inayolingana na kiwango cha hatari kama sehemu ya Utiifu wa sera za KYC na AML, Paxful imechukua hatua zifuatazo:

  • Kuteua Ofisa Mkuu wa Masuala ya Utiifu ambaye ana uhuru na uzoefu wa kiwango cha kutosha, aliye na wajibu wa kusimamia masuala ya utiifu kwa kutumia sheria na kanuni zinazohusiana na mwongozo wa sekta;
  • Kuanzisha na kudumisha sera ya KYC inayolingana na kiwango cha hatari, Ukaguzi wa Wateja (CDD) na Ukaguzi wa Kina (EDD);
  • Kuanzisha viwango vinavyolingana na kiwango cha hatari kwa uthibitishaji wa watumiaji wa Kampuni (soma chapisho hili la Blogu);
  • Kushirikiana na maombi ya mamlaka ya utekelezaji wa sheria na masharti ya sheria za nchi;
  • Kujaza Ripoti za Shughuli Zisizo za Kawaida (“SAR”);
  • Kutoa mafunzo ya BSA/AML/OFAC kote kwenye kampuni;
  • Kutumia mifumo mbalimbali ya kuzuia ulaghai;
  • Ufuatiliaji endelevu wa shughuli ya ununuzi na uuzaji unaolingana na sheria;
  • Kutekeleza uchunguzi kwa kutumia takwimu za mitandao husika;

Tunajaza SAR ikiwa tunajua, tunashuku au tuna sababu ya kushuku kuwa shughuli zisizo za kawaida zimetendeka kwenye mfumo wetu. Shughuli ya ununuzi na uuzaji zisizo za kawaida mara nyingi huwa ni shughuli ambazo hazilingani na biashara halali na inayojulikana ya mtumiaji, shughuli za kibinafsi au utendakazi wa kibinafsi. Ofisa wetu Mkuu wa Masuala ya Utiifu hukagua na kuchunguza shughuli zisizo za kawaida ili kubaini ikiwa maelezo ya kutosha yamekusanywa ili kuthibitisha hatua ya kujaza SAR. Ofisa wetu Mkuu wa Masuala ya Utiifu huhifadhi rekodi na hati za ziada za SAR zote ambazo zimejazwa.

Kampuni pia imeiga sera na taratibu za vikwazo vya OFAC zinazotumika, zilizobuniwa ili kulinda mfumo dhidi ya kutumiwa kwa shughuli za ununuzi na uuzaji ambazo haziruhusiwi na watu waliowekewa vikwazo au kwa madhumuni ya kukwepa au kuepuka vikwazo vya Marekani na vya kimataifa.

Paxful inashirikiana kikamilifu na orodha zote za vikwazo za OFAC, Wananchi Maalum Waliotengwa (SDN) na watu Waliozuiliwa. Tafadhali rejelea kiungo kifuatacho ili upate orodha ya Kampuni ya nchi zilizopigwa marufuku kulingana na kiwango cha hatari ambazo zimezuiwa kutumia mfumo wa Paxful.

Iwapo Paxful imekupatia tafsiri ya toleo la lugha ya Kiingereza la sera hii, basi unakubali kuwa umepewa tafsiri hiyo kwa ajili ya kukurahisishia mambo tu na kuwa toleo la lugha ya Kiingereza la sera hii litasimamia uhusiano wako na Paxful. Ikiwa kuna utofauti wowote baina ya maelezo ya toleo la lugha ya Kiingereza na tafsiri, basi toleo la lugha ya Kiingereza litatumika.