Kuwa sehemu ya mfumo ambao unakusaidia kujenga nguvu zako, na upate mashirika yenye shauku unayoweza kushirikiana nayo yenye mawazo sawa na yako. Kusanyeni nyenzo zenu, mkishiriki maono yenu, fanyeni kazi pamoja, na mjenge mambo makubwa kwa ajili ya jamii zenu.
Tufanye kazi pamojaKwa nini unapaswa kujiunga na Ushirika wa Paxful?
Tunaleta pamoja mashirika na watu binafsi kutoka tabaka mbalimbali. Biashara, watu binafsi na mashirika yasiyo ya faida wote wanaweza kushirikiana katika malengo na maono yao shirikishi kwa ajili ya jamii zao. Kuna faida nyingi kutokana na ushirikiano huu:
Pata watu wengine wenye mtazamo kama wako na uguse maisha zaidi kwa kazi yenye maana unayoipenda na inayoshughulikia jamii.
Shiriki katika kampeni ya Mahusiano na usambaze neno kuhusu chapa yako zadi ya hapo awali.
Toa elimu kuhusu bidhaa au biashara zako katika maeneo mapya na uwe mstari wa mbele katika kuunda sera kuhusu kazi yako.
Ungana na wengine dhidi ya washindani na waache ukiwatazama katika kioo cha kuonyesha nyuma. Umoja ni nguvu.
Tafuta msaada unaofaa ili kuifanya biashara yako ifuate sheria za nchi katika masoko mapya.
Nenda katika ngazi ya kimataifa, ingia katika masoko mapya, na ufikie wateja wengi zaidi wa bidhaa na huduma zako.
Yote hayo ni mazuri, lakini bado huna uhakika utafaa katika sehemu gani? Iwe uko katika sekta ya teknolojia ya fedha au ufadhili, Ushirika wa Paxful upo kwa ajili yako. Hizi hapa ni namna tofauti za wewe kushiriki na kunufaika.
Saidia kuelimisha jamii kuhusu habari mpya juu ya sarafufichwa na teknolojia
Leta mabadiliko katika dunia ya fedha kwa mawazo yako ya ubunifu na utengeneze bidhaa nzuri ambazo zitajenga taswira ya usoni ya pesa.
Zambaza neno lako duniani kote, kwa ujumbe sahihi, ukifika mbali kuliko hapo awali
Pambana na changamoto mbalimbali katika sekta ya sarafufichwa, gundua masoko na fursa mpya
Ongoza kundi katika michezo ya video na burudani ya sarafufichwa. Huisha mawazo yako yote mazuri ya michezo ya video.
Kingine chochote unachotaka ushiriki pia. Huwezi kujua mawazo yako yataweza kumpa hamasa mtu yupi!