Vigezo vya Huduma vya Programu Shirikishi

Tarehe ya kuanza: Oktoba 21, 2019

Asante kwa kujisajili kama mwanachama wa Programu Shirikishi ya Paxful. Taarifa ulizotoa kwa Paxful kama sehemu ya mchakato wa usajili zitachambuliwa na kufanyiwa kazi na Paxful kulingana na Sheria za Jumla za Ulinzi wa Data za Umoja wa Ulaya ("GDPR"). Sera ya Faragha ya GDPR ilikubaliwa nawe kama sehemu ya mchakato wa usajili wa Mshirika.

Kwa kuendelea kutumia tovuti ya Paxful (iwe ni kama Mshirika au vinginevyo), itachukuliwa kuwa umekubali Sera ya Faragha, ikiwa ni pamoja na jinsi inavyoweza kuwa kila wakati inabadilishwa, inaongezewa au inafanyiwa marekebisho. Toleo la sasa la Sera ya Faragha linaweza kufikiwa kutoka kwenye ukurasa wa Mwanzo wa tovuti hii au kwa kubofya kiungo hiki: https://paxful.com/privacy. Ili kuepuka mashaka, tafadhali tambua kwamba baadhi ya taarifa za akaunti zinaweza kushirikiwa na Washirika wako kama sehemu ya ushiriki wako kwenye Programu Shirikishi, ikijumuisha pasipo ukomo maelezo ya eneo lako na shughuli za akaunti.

Vifuatavyo ni Vigezo na Masharti yanayotumiwa na Programu Shirikishi. Paxful ina haki (katika nafasi yake na pasipo kutoa notisi ya awali) ya: (a) kubadili mojawapo au Vigezo na Masharti yote, wakati wowote na mara kwa mara, ikijumuisha (pasipo ukomo) kubadili asilimia ya sehemu ya faida iliyoelezewa hapa chini, (b) kusimamisha au kughairi Programu Shirikishi, na/au (c) kusimamisha au kusitisha kabisa akaunti yako ya Programu Shirikishi na ya Paxful ikiwa utajihusisha na vitendo vilivyoelezwa hapa chini.

Kama Mshirika, una fursa ya kuwaalika watu wengine kwenye Soko la Bitcoin la Paxful na kupata kiasi cha faida kulingana na uchuuzi wao wa BTC wanaoufanya kwenye jukwaa. Paxful inawalipa Washirika wote sehemu ya faida kwa BTC tu.

Programu Shirikishi imeundwa kama programu ya viwango viwili inayotumika kwa watumiaji wengine wapya tu:

 • Washiriki wa Kiwango cha 1
  Mshiriki wa Kiwango cha 1 ni mtumiaji mwingine ambaye anajisajili kutumia Soko la Bitcoin la Paxful kwa kutumia kiungo cha kipekee cha kujisajili ambacho Paxful ilikitoa kwako ulipojiunga kwenye Programu Shirikishi.
 • Washiriki wa Kiwango cha 2
  Mshiriki wa Kiwango cha 2 ni mtumiaji mwingine ambaye anajisajili ili kutumia Soko la Bitcoin la Paxful kwa kutumia kiungo cha kipekee cha kujisajili ambacho Paxful itakuwa ilikitoa kwa Mshiriki wako wa Kiwango cha 1.

Kiasi cha faida kinacholipwa.

Isipokuwa vinginevyo na ilivyokubaliwa na Paxful, utapata kiasi cha faida kutoka Paxful kila wakati Mshiriki wa Kiwango cha 1 au cha 2 anapokamilisha muamala wa "Kununua" BTC kwa kutumia Paxful.

Kama unavyofahamu, Paxful inatoza Ada ya Eskro kwa kila uchuuzi unaokamilishwa kwenye jukwaa lake. Ada ya Eskro inaweza kubadilishwa na Paxful wakati wowote na mara kwa mara. Unaweza kupata ufafanuzi wa Ada ya Eskro na kiasi chake cha sasa kwa kubofya kiungo hiki: https://paxful.com/support/en-us/articles/360013609793-Paxful-fees

 • Mshiriki wa Kiwango cha 1 anapokamilisha muamala wa "Kununua" BTC kwa kutumia Paxful, Paxful itaongeza salio kwenye Pochi yako ya Washirika (katika BTC) sawa na 50% ya Ada Inayotumiwa ya Eskro.
 • Mshiriki wa Kiwango cha 2 anapokamilisha muamala wa "Kununua" BTC kwa kutumia Paxful, Paxful itaongeza salio kwenye Pochi yako ya Washirika (katika BTC) sawa na 10% ya Ada Inayotumiwa ya Eskro.
 • Hata hivyo, kama Mshirika wako wa Kiwango cha 1 ataanzisha muamala wa "Kununua" BTC na Mshirika wa Kiwango cha 1 wa mwanachama mwingine wa Programu Shirikishi, basi kila mmoja wenu na mwanachama huyo mwingine mtagawana kwa usawa kiasi cha faida cha 50%.
 • Hata hivyo, kama Mshirika wako wa Kiwango cha 2 ataanzisha muamala wa "Kununua" BTC na Mshirika wa Kiwango cha 2 wa mwanachama mwingine wa Programu Shirikishi, basi kila mmoja wenu na mwanachama huyo mwingine mtagawana kwa usawa kiasi cha faida cha 10%.
 • Wakati wowote unaponunua au kuuza kwa mmoja wa Mshirika wako wa Kiwango cha 1 au cha 2 hautapata kiasi chochote cha faida.

Kiasi chako cha faida kilichopatikana kutoka kwenye mauziano yoyote kama hayo kitaongezwa kwenye Pochi yako ya Washirika mara tu baada ya muamala huo kukamilika. Kila wakati mauziano kama hayo yanapokamilika, Paxful itakutumia barua ya uthibitisho. Kwa namna hii, unaweza kutazama salio la Pochi yako ya Washirika likikua kwenye dashibodi yako ya Paxful.

Wakati mwingine, unaweza pia kuwa na sifa ya kupata ada ya ushirikishaji kila wakati Mshiriki wako wa Kiwango cha 1 au cha 2 anapokamilisha muamala wa "Kuuza" BTC kwa kutumia Paxful. Ili kutathmini uhalali wako wa kupata ada kutokana na mauziano ya "Kuuza" ya Mshirika wako wa Kiwango cha 1 na cha 2, tafadhali wasiliana na timu ya usaidizi ya Paxful kwa [email protected]. Paxful ina haki ya kutathmini, jinsi itakavyo na ionavyo, kama unaweza kuruhusiwa au kukataliwa kupata ada yoyote ya ushirikishi kwa muamala wa "Kuuza".

Kutoa Kiasi Chako cha Faida

Pale salio katika Pochi yako ya Washirika linapofikia angalau US$10 (katika thamani ya BTC), utaweza kutuma salio lote kwenda kwenye Pochi yako ya Paxful ya BTC. Pindi salio la Pochi yako ya Washirika linapofikia thamani ya juu ya US$ 300, utaombwa kuwasilisha uthibitisho wako wa utambulisho na anwani. Baada ya kufanya hivi, unakuwa huru kufanya chochote kwa kutumia mapato uliyonayo. Kwa kutupatia taarifa hii au taarifa zozote ambazo zinaweza kuwa zinahitajika, unathibitisha kwamba taarifa zote ni sahihi, kweli na sio za kupotosha. Unakubali kutuarifu haraka ikiwa kuna mabadiliko ya taarifa yoyote uliyotupatia. Unatupa idhini ya kufanya maulizo iwe ni moja kwa moja au kwa kupitia kwa mtu mwingine, tunayofikiri ni muhimu katika kukuthibitisha utambulisho wako au kukulinda wewe na/au sisi dhidi ya ulaghai, au kosa lolote la jinai la kifedha, na kuchukua hatua tunazofikiri ni za muhimu kulingana na majibu ya maulizo hayo. Tunapofanya maulizo haya, unatambua na kukubali kwamba taarifa zako binafsi zinaweza kuwekwa wazi kwa mamlaka za mikopo na uzuiaji wa ulaghai au mamlaka za uchunguzi wa makosa ya jinai ya kifedha na kwamba mamlaka hizi zinaweza kujibu maulizo yetu kikamilifu.

Kidokezo Kikuu: Tunapendekeza uuze mapato yako ya BTC kwenye jukwaa letu kwa faida zaidi.

Vitendo Visivyokubalika

Ifuatayo ni orodha ya uwakilishi (lakini sio pekee) ya aina ya vitendo na tabia ambazo zinaweza kupelekea Paxful (kama ilivyowekwa na maamuzi na hukumu binafsi ya Paxful) (a) kughairi au kudai tena malipo ya Kiasi chako cha Faida (iwe kimetolewa au la), na/au (b) kusimamisha au kusitisha kabisa akaunti yako ya Programu Shirikishi na ya Paxful.

 • Kutumia barua taka kuwavutia watu kuingia kwenye jukwaa la Paxful.
 • Kujihusisha na vitendo vyovyote vilivyo kinyume na sheria, iwe vinahusiana na matumizi yako ya jukwaa la Paxful na huduma zake au la.
 • Kufungua akaunti ya ziada kwenye jukwaa la Paxful inayofaidika na Programu Shirikishi kwa namna yoyote. Unaruhusiwa kuwa na akaunti moja pekee na huruhusiwi kuuza, kukopa, kushiriki au kufanya akaunti yako ipatikane au maelezo yoyote yanayohitajika ili watu au huluki zingine kando na wewe ziweze kufikia akaunti yako. Huruhusiwi kabisa kuweka maelezo ya uongo kwa akaunti yako, kudanganya kuhusu nchi yako ya asili au kutoa hati za uongo za vitambulisho.
 • Uvunjaji au ukiukaji wowote wa mojawapo ya wajibu wako chini ya Vigezo na Masharti haya kwa upande wako au mwakilishi wako.
 • Matumizi ya – kwa namna yoyote ya kutangaza au habari yoyote au taarifa ya aina yoyote ambayo utaianzisha au kuihabarisha au kuidhibiti – maneno "pax" au "paxful" au mengine yanayofanana, kusikika kama hayo, au maneno mengine, alama, au chapa ambazo Paxful itadai kuwa zinachanganya kwa kufanana na chapa yake ya biashara ya PAXFUL.
 • Kudharau, kusingizia, au kukashifu (a) Paxful au wakurugenzi, maofisa, wafanyakazi, wakandarasi, mawakala, au wawakilishi wake, au (b) watumiaji wa jukwaa la Paxful, ikijumuisha wanachama wengine wa Programu Shirikishi.
 • Kujihusisha katika vitendo vyovyote ambavyo Paxful inaamini (kwa mtazamo na jinsi inavyoamua yenyewe) vinaweza kuiletea matatizo ya kisheria, kikanuni, au taratibu za nchi yoyote, vyombo vya kimataifa (ikijumuisha Umoja wa Ulaya), au mamlaka mengine au mamlaka ya kiserikali ikijumuisha, pasipo ukomo kamari haramu, ulaghai, utakatishaji fedha, au vitendo vya kigaidi.
 • Kujihusisha na vitendo vyovyote vilivyo kinyume na sheria, iwe vinahusiana na matumizi yako ya jukwaa la Paxful na huduma zake au la.
 • Kutoa taarifa za uongo, zisizo sahihi, au zinazopotosha.
 • Kutoa taarifa za uthibitisho wa utambulisho na anwani zilizo za uongo, zisizo sahihi, au zinazopotosha.
 • Kuhimiza au kushawishi mtu mwingine yeyote kushiriki kwenye shughuli zozote ambazo haziruhusiwi chini ya Kifungu hiki.

Haki za Uvumbuzi

Isopokuwa vinginevyo na ilivyoonyeshwa na sisi, haki zote za uvumbuzi katika tovuti na katika maudhui yoyote yanayotolewa kuhusiana na huduma zetu, ni mali ya Paxful na watoa vibali au wasambazaji wetu na zinalindwa na sheria zitumikazo kulinda haki za uvumbuzi. Hatutoi leseni yoyote kwa matumizi ya maudhui yoyote kwenye tovuti. Huwezi kuuza au kubadilisha nyaraka za Tovuti au kuzalisha upya, kuonyesha, kufanyia vitendo hadharani, kusambaza au kutumia nyaraka kwa namna yoyote kwa malengo yoyote ya kibiashara au umma. Matumizi yako ya nyaraka katika tovuti nyingine yoyote au kwenye huduma inayofanana na ya kushiriki mafaili kwa lengo lolote hairuhusiwi.

Huwezi kunakili nyaraka zozote au maudhui yaliyo kwenye Tovuti au yanayofikiwa kwenye Tovuti bila ruhusa yoyote ya maandishi. Haki yoyote ambayo haijatolewa ruhusa ya matumizi ya nyaraka zilizojumuishwa kwenye Tovuti ni mali kamili ya Paxful.

Kima cha Wajibu/Kanusho

Tovuti hii na Programu Shirikishi zinatolewa kwa msingi wa "kama ilivyo" na "kama inavyopatikana" kwa ajili ya taarifa na matumizi yako bila uwakilishi ama pendekezo lolote. Kwa kiwango cha juu zaidi kinachoruhusiwa na sheria, hatutoi dhamana yoyote iwe ni ya tamko au maelezo, kuhusiana na tovuti au Programu Shirikishi, ikijumuisha pasipo ukomo, dhamana ya maelezo ya ubora wa kuridhisha, utendaji, uimara kwa kusudi fulani, kutokiuka, utangamo, ulinzi, usahihi, hali au ukamilifu, au dhamana ya maelezo inayotokana na sababu ya kuhusiana au kutumia au kuchuuza.

Ikiwa na katika kiwango cha juu zaidi kinachoruhusiwa na sheria, hatutawajibika kwa ajili ya:

 • 1. hasara yoyote ya kiuchumi (ikijumuisha hasara ya mapato, faida, mikataba, biashara au akiba iliyotegemewa);
 • 2. hasara ya nia njema au sifa;
 • 3. Hasara zozote mahsusi au zisizo za moja kwa moja au za madhara, vyovyote inavyojitokeza.

Malipo na Kutokuathiriwa

Unakubali kutowajibisha Paxful, Inc (na kila moja ya maofisa, wakurugenzi, wanachama, wafanyakazi, mawakala na washirika) kwa madai, mahitaji, vitendo, uharibifu, hasara, gharama, ikijumuisha pasipo ukomo ada za huduma za kisheria, zinazotokana au kuhusiana na: matumizi yako ya, au vitendo vinavyohusiana na, Programu yetu Shirikishi; au ukiukaji wako wa Vigezo na Masharti haya. Aidha, unakubali kwamba utawajibika kikamilifu kwa (na kututetea kikamilifu dhidi ya) madai yote, wajibu, uharibifu, hasara, gharama, ikijumuisha ada za huduma za kisheria, zilizotuathiri ama zilizojitokeza kutokana na uvunjaji wowote wa Vigezo na Masharti uliofanywa na wewe au wajibu wowote uliobebwa na sisi kutokana na matumizi yako ya huduma au Programu Shirikishi, au matumizi ya mtu mwingine yoyote anayefikia huduma kwa kutumia akaunti yako, kifaa au akaunti ya ufikiaji wa mtandao; au ukiukaji wako wa sheria na haki zozote za mtu meingine yeyote.

Jumla

Vigezo na Masharti haya na matumizi yako ya Tovuti na Programu Shirikishi vitaongozwa na kuendeshwa kulingana na Sheria za Marekani. Mashtaka yoyote yanayotokea kutokana na Vigezo na Masharti haya au matumizi yako ya Tovuti na Programu Shirikishi yatasuluhishwa katika Mahakama za Marekani. Hakuna chochote katika Vigezo na Masharti haya kitakachopelekea kuathiri haki zako za kisheria kulingana na Sheria za Marekani. Ikiwa sehemu yoyote ya Vigezo na Masharti haya itazingatiwa kuwa haitumiki au haiwezi kutekelezwa kikamilifu au kwa sehemu yake na mahakama yoyote ya Marekani, uwezo wa kutumika au kutekelezwa kwa vifungu vingine vya vigezo na masharti haya hautaathirika. Vichwa vyovyote vilivyo kwenye Vigezo na Masharti haya vimekusudiwa kwa madhumuni ya kutoa maelezo pekee na si vifungu vinavyoweza kutekelezwa vya Vigezo na Masharti haya.