Paxful inabadili ulimwengu wa fedha. Ndani ya miaka mitano tu, tumekuwa moja ya masoko yanayoongoza ya mtu kwa mtu ya bitcoin tukitumiwa na mamilioni ya watu duniani kote. Na ndiyo kwanza tunaanza.
Paxful ilianza kwa lengo rahisi: kuwawezesha watu bilioni nne wasiotumia au wasiofikiwa na huduma za benki, ili waweze kuwa na udhibiti wa pesa zao kwa njia ambayo hawakuwahi kuwa nayo hapo awali.
Ray Youssef, Mkurugenzi Mkuu
Ray, mhamiaji kutoka Misri aliyekulia katikati ya New York, mara zote alikuwa na shauku ya kusaidia watu wengine. Alikuwa na ndoto ya dunia ambamo fedha ilifikia kila mtu na wazo hilo lilidhihirika kama Paxful.
Tunaishi na kufanya kazi kwa maadili matatu rahisi ili kutuongoza katika safari yetu kuu.
Kuwa Shujaa
Hapa Paxful, tunatumia juhudi zaidi ya zile za kibinadamu kufanikisha kazi. Tunafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa ndoto za watumiaji wetu zimetimia. Tunafanya yasiyowezekana kuwa uhalisia ili kubadili maisha ya mabilioni ya watu duniani kote.
Jenga kwa ajili ya Watu
Tunapofanya maamuzi hapa Paxful, tunawafikiria watu—si faida. Tunafikia sehemu ambazo dunia nzima imezipuuzia na kuzisahau. Tunasaidia familia kustawi, kujenga mashule, na kuwawezesha watumiaji wetu kuwa mabosi wao wenyewe.
Endelea Kuunganishwa Mitaani
Tunasikiliza jamii yetu wakati wowote hapa Paxful. Hatuko maghorofani na "suti"—tuko mitaani na watu. Mara zote tunazungumza na watumiaji wetu, tukiwauliza maoni yao, na kujenga kitu bora zaidi.
Paxful inabadili jinsi dunia inavyohamisha fedha na inaendekeza sarafufichwa - ikiruhusu utumaji kwa kila mtu, popote, wakati wowote.
Huna akaunti ya benki? Hakuna tatizo. Tuna zaidi ya njia 300 za malipo unazoweza kuchagua, na kuifanya iwe rahisi kwako kuhamisha fedha zako jinsi unavyotaka.
Teknolojia Inayowezeshwa na Watu
Paxful inafanya kazi katika mtindo wa mtu kwa mtu, ikimaanisha kwamba watumiaji wetu wanachuuza na watu halisi—jinsi bitcoin ilivyokusudiwa kutumika.
Pochi ya Sarafufichwa Bila Malipo
Unaweza kuitegemea, ni rahisi-kutumia na haigharimu chochote. Pochi yetu ya kidijitali inampa kila mtu mahali salama pa kuhifadhi utajiri wake — haijalishi wewe ni nani au unatoka wapi.
Yenye Ulinzi
Usalama na ulinzi ni vitu muhimu zaidi unaposhughulikia pesa zako. Biashara zote kwenye Paxful zimelindwa na huduma yetu ya eskro salama ili kuondoa wasiwasi.
Hapa Paxful, tunaamini kwamba Bitcoin ndiyo suluhisho la siku zijazo na chombo cha mabadiliko. Built with Bitcoin ni mkakati wetu wa kutoa fursa, kuboresha maisha, na kuifanya dunia kuwa mahali pazuri kwa jamii ambazo zinaihitaji zaidi, kwa kutumia Bitcoin.
Lengo? Kujenga shule 100, vituo vya maji, na shule za ujasiriamali zinazofadhiliwa kwa ukamilifu na Bitcoin. Kwa sasa tunajenga shule yetu ya nne na bado tunazo 96 zilizobaki!
Built with Bitcoin pia ilisaidia kutoa misaada dhidi ya athari za COVID-19 barani Afrika—kupitia michango kutoka kwa watumiaji na rafiki zetu, tuliweza kutoa chakula, vieuzi na vifaa vingine vya kujilinda kwa wale wanavihitaji.
Jiunge nasi! Tuibadilishe dunia pamoja.
Pata Maelezo ZaidiOfisi duniani kote
Wafanyakazi ambao wanataka kuifanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi
Lugha zinazozungumzwa katika ofisi zetu za kimataifa
Lengo la kujenga dunia yenye ufikiaji sawa wa kifedha kwa wote
Ikiwa una tatizo linalohitaji usaidizi au unataka kutoa maoni kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha bidhaa zetu, tungependa kusikia zaidi kuhusiana na hilo . Hata hivyo, kama unataka kuwasiliana na Paxful kuhusu mambo mengine yanayohusiana na biashara, tunapatikana pia kupitia njia nyingine za mawasiliano.
Habari na Mauzo
Saidia kusambaza neno kuhusu Paxful katika vyombo vya habari na njia zingine za matangazo. Wasiliana nasi kwa maulizo ya habari kupitia [email protected].
Zawadi ya Kuripoti Hitilafu
Programu ya Utambuzi wa Kasoro inakupa fursa ya kupata zawadi ya kutambua matatizo ya kiufundi. Toa taarifa kupitia [email protected]. Kwa maelezo zaidi bofya hapa.
Akaunti za Biashara
Ili kusajili akaunti ya biashara kwa ajili ya biashara za uchuuzi kwenye Paxful, unaweza kutuma barua pepe kwa [email protected]. Kwa maelezo zaidi bofya hapa.
Mauzo na Ubia
Ili kuulizia kuhusu kuwa mshirika. Tufahamishe ikiwa unataka kuwa mshirika nasi kwa kututumia barua pepe kwa [email protected].
Unda akaunti yako mwenyewe ya Paxful na uchukue hatua kwenye dunia ya sarafufichwa.